Kwa maudhui

Maneno kaj, , sed, plus, minus kaj nek ni viunganishi. Kuhusu nek soma maelezo kuhusu ukanushaji.

Kaj

Kaj huunganisha mambo mawili, ambayo yana jukumu moja katika sentensi:

 • Karlo kaj Petro manĝas. - Karlo na Petro wanakula.

  Watu wawili wanafanyaa vitendo vimoja.Kuna viima viwili.

 • Karlo manĝas kaj trinkas. - Karlo anakula na kunywa

  Karlo anafanya vitendo viwili(wakati huo huo au mfululizo). Kuna prediketo mbili.

 • Karlo manĝas rizon kaj legomojn. - Karlo anakula wali na mchicha.

  Mambo mawili yanaathiriwa na hatua moja kwa njia ile ile. Kuna shamrisho mbili za aina moja.

 • Petro manĝas per forko kaj tranĉilo. - Petro anakula kwa kisu na kijiko.

  Vifaa viwili vinasaidia katika kitendo kimoja, unaweza kurudilia kihusishi:per forko kaj per tranĉilo.

 • Petro estas maljuna kaj saĝa. - Petro ni mkubwa na mwenye busara.
 • Petro havas grandan kaj luksan domon. - Petro ana nyumba kubwa na ya kifahari.

  Wakati vivumishi viwili ni wasifu wa nomino moja, mara nyingi kaj inaondolewa: Petro anamiliki nyumba kubwa na yakifahari.

 • Karlo laboras por kaj per Esperanto. = ... por Esperanto kaj per Esperanto. - Karlo hufanya kazi kwa ajili ya na kwa kutumia Kiesperanto ya Kiesperanto. = kwa ajili ya Kiesperanto na kwa kutumia Kiesperanto.
 • Petro legis la gazeton, kaj Karlo rigardis televidon. - Petro alisoma gazeti, na Karlo anatazama TV.

  Vichazi huru viwili.

 • Ili diris, ke ili tre amuziĝis, kaj ke ili volonte revenos venontjare. - Walisema walikuwa na furaha nyingi, na wangefurahi kurudi mwaka ujao.

  Vifungu viwili vya kesentensi.

 • Jen venas tiu knabino, kiu savis mian vivon, kaj kiu poste malaperis. - Hapa huja msichana alieokoa maisha yangu,na baadae alipotea.

  Vifungu viwili na kiu.

Tunapozungumzia mambo zaidi ya mawili yaliyo na jukumu moja, kawaida kaj tu pili mwisho, hasa wakati kuna orodha ndefu ya vitu. Ambapo hakuna kaj unaweza kusimama wakati unapozungumza. Kwa kuandika unaweka mkato:

 • Petro, Karlo, Elizabeto kaj Eva vojaĝis kune al la kongreso. = Petro kaj Karlo kaj Elizabeto kaj Eva vojaĝis... - Petro, Karlo Elizabeti na Eva walienda pamoja kwenye kongamano. = Petro na Karlo na Elizabeti na Eva walienda ...
 • Hodiaŭ ni manĝos supon, salaton, viandaĵon, frititajn terpomojn kaj glaciaĵon. - Leo tutakula supu, saladi, nyama, viazi vya kukaanga na ice cream.
 • Li iras per aŭto, ŝi iras per trajno, kaj mi iras piede. - Anaenda kwa gari, anaenda kwa garimoshi,na ninaenda kwa miguu.

Katika staili ya msemo, kunakipindi tunaacha ​kaj:

 • Li estas stulta, malaminda. Mi tute ne ŝatas lin. - Yeye ni mjinga na mwenye karaha. Simpendi kabisa yeye.
 • Venis Karlo, Petro, Eva. Jes, ĉiuj miaj amikoj venis. - Karlo,Petro na Eva walikuja. Ndiyo,marafiki zangu wote walikuja.

Kwa msisitizo na kung'ang'ania unaweza kutumia kaj kabla ya kila kitu, pia kabla ya kwanza .

Tofauti ya uhusiano kati ya sentensi zilizounganishwa

Wakati sentensi zinaunganishwa kwa kaj, uungaji huu unaweza kuwakilisha mahusiano mbalimbali na maana mbalimbali. Ili kuelewa ni uhusiano gani, tunapaswa kutegemea mazingira:

 • Mi lavis la vestaĵojn, kaj (poste) mi sekigis ilin. - Nilifua nguo,na (baadae)nilizianika.

  Kaj huonyesha wa wakati wa mfululizo. Neno post (baadaye) linaweza kutumika, kama linahitajika, kusaidia kuelewa.

 • Anno estas gaja persono, kaj (kontraste) Elizabeto estas silentema. - Anne ni mtu mwenye furaha, na (ulinganuzi) Elizabeth ni mkimya.

  Kaj kinaonyesha ulinganuzi.

 • Ŝi havas brunajn okulojn, kaj (aldone) ŝiaj haroj estas longaj. - Ana macho ya njiwa,na (katika kingine)ana nywele ndefu.

  Kaj huonyesha ongezeko la taarifa.

inafanya kazi kama kaj . Inaweza kuunganisha vitu sawa kwa njia ile ile, lakini inaonyesha kwamba vitu vinavyohusishwa ni mbadala . inaonyesha kwamba mtu anaweza kufanya chaguo kati ya vitu vinavyohusishwa, au kwamba haijulikani kuwa mmoja wao ni sahihi:

 • Petro Karlo laboras. - Pita au Karlo wanafanya kazi.

  Viima viwili vinavyowezekana. Kimoja wapo kinafanya kazi, na vyote.

 • Ni povas manĝi viandaĵon fiŝaĵon. Kion vi preferas? - Tunaweza kula nyama au samaki? Wewe unapendelea nini?

  chaguo kati ya shamrisho kitondo mbili.

 • Vi devas fari tion per fosilo (per) hakilo. - Unapaswa kufanya hivyo na jembe au na shoka.
 • Ĝi estis ruĝa flava. Mi ne memoras klare. - Ilikuwa nyekundu au njano . Sikumbuki vizuri.
 • Mi konstruus lignan ŝtonan domon. - Ningejenga nyumba ya mbao au mawe.
 • Ĉu eblas konstrui aŭton kun kvin ses radoj? - Inawezekana kujenga gari yenye tairi Tano au sita?
 • La kato troviĝas sur sub la domo. - Ni paka yupo juu au chini ya nyumba.
 • Ĉu mi kapablas plenumi tiajn laborojn ĉu mi ne kapablas? - Ninaweza kutekeleza kazi hizo au siwezi?
 • Ŝi ne sciis, ĉu ŝi nur sonĝis ĉu tio estis efektivaĵo. - Yeye hakujua kwamba alikuwa anaota tu aukwamba ilikuwa ni kweli.
 • La pasantoj forflankiĝis antaŭ ŝi, supozante, ke ŝi estas frenezulino ke ŝi havas ian urĝegan bezonon rapidi. - Waliopita wamesimama, wakidhani kuwa wazimu au kwamba ana dharula aende haraka
 • Glaso de vino estas glaso, en kiu antaŭe sin trovis vino, kiun oni uzas por vino. - Bilauli ya divai ni blauli ambayo imetumiwa kwa divai hapo awali, au ambayo hutumiwa kwa divai.
 • Vi povas vojaĝi per trajno, buso, aŭto biciklo. - Unaweza kusafiri kwa gari moshi,basi,gari au baiskeli.
 • Kiu povas helpi min? Eble Karlo, Petro Elizabeto. - Nani anaweza kunisaidia mimi? Labda Karlo,Pita au Elizabeti

Kwa kawaida ni ya kipekee. Hii ina maana kwamba moja tu ya njia mbadala inaweza kuwa halali. Mara kwa mara hata hivyo ni jumla. Kisha inakuwezesha kuchagua zaidi ya njia moja (labda hata zote). Ikiwa ni jumuishi au ya kipekee, inaonyesha mazingira. Ili kusisitiza kuwa } ni ya kipekee, mtu anaweza kutumia kabla ya kila mbadala . Ili kuonyesha kwamba inajumuisha, wakati mwingine, hasa katika lugha iliyoandikwa, kutumia maneno na/aŭ: Safari itafanyika kwa treni { 7} na/aŭ basi . = Safari itafanyika kwa basi ya treni au , au kwa treni na . { 2} Safari itafanyika kwa treni basi au vyote viwili. Kwa kawaida, haitumii kaj/aŭ katika lugha ya kusema, kwa kuandika tu. Inaonekana kustahili kuepuka kaj/aŭ pia katika matumizi yaliyoandikwa. Ni bora kuongoza fursa ya kuchagua njia zote.

Sed

Kiunganishi sed (lakini) huunganisha sentensi au kifungu, huku kikionyesha tofauti kati yao:

 • La papero estas tre blanka, sed la neĝo estas pli blanka. - Karatasi ni nyeupe sana, lakini theruji ni nyeupe zaidi.
 • Li amas min, sed mi lin ne amas. - Hunipenda mimi,lakini mimi simpendi.
 • Mi zorgas pri ŝi tiel, kiel mi zorgas pri mi mem; sed ŝi mem tute ne zorgas pri si kaj tute sin ne gardas. - Ninamjali kama ninavyojijali mwenyewe; lakini yeye hajijali mwenyewe na hajilindi ata kidogo.
 • Nia provincestro estas severa, sed justa. - Mkuu wa mkoa ni mkali, lakini ni mkweli.
 • Mi volis lin bati, sed li forkuris de mi. - Nilihitaji kumpiga ,lakini alikimbia mbali nami.
 • Mi kriis tiel laŭte, kiel mi povis, sed neniu min aŭdis, mi estis tro malproksime. - Nilipiga kelele niwezavyo, lakini hakuna mtu aliyenisikia. Nilikuwa mbali sana.
 • La patro ne legas libron, sed li skribas leteron. - Baba hasomi kitabu,lakini yuko anaandika barua.
 • Tio ĉi estis jam ne simpla pluvo, sed pluvego. - Hii haikuwa mvua ya kawaida, lakini mvua kubwa .
 • Anstataŭ kafo li donis al mi teon kun sukero, sed sen kremo. - Badala ya kahawa alinipa chai ya sukari, lakini bila ya mtindi.

  Walidhani kwamba pia kutakuwa mtindi katika chai.

Sed mara nyingi huonekana pamoja na tamen , ambayo inasisitiza utofauti:

 • Mi ne scias la lingvon hispanan, sed per helpo de vortaro hispana-germana mi tamen komprenis iom vian leteron. - Sifahamu Kihispania, lakini kwa msaada wa kamusi ya Kihispania-Kijerumani nilielewa barua yako kwa kiasi fulani.
 • Ŝi havis forton kaj ŝi estis laborema, sed ŝi tamen restis malriĉa. - Alikuwa na nguvu na alikuwa mwenye bidii, lakini alibakia masikini.

Wakati wa kutumia tamen mtu anaweza kutumia kaj badala ya sed, kwa sababu tofauti inaelezwa wazi na tamen:

 • Li havis la impreson, ke li sonĝas kaj tamen ne sonĝas. - Alikuwa na hisia ya kwamba alikuwa akiota, lakini hakukuwa anaota.
 • La lekanto sentis sin tiel feliĉa, kvazaŭ tiam estus grava festotago, kaj tamen tiam estis nur simpla lundo. - Mlambaji alifurahia kama ilikuwa ni siku ya likizo, ila ata hivyo ilikuwa ni jumatatu tuu ya kawaida.

TamenKwa kawaida ni adjuct, wakati sed ni kiunganishi. Kwa sababu hiyo sed inakuja mwanzo wa sentensi wakati tamen inaweza kuonekana katika nafasi mbalimbali ndani ya sentensi. Wakati mwingine tamen inaonekana mwanzo wa kifungu kikuu. Katika hali hiyo tamen inachukua nafasi ya mwanzo katika kishazi huru. Tamen wakati huo ni sawa na sed. Mtu anaweza pia kusema kuwa sed au kaj hazisikiki vizuri: Ana hasira nyingi na anakasirishwa na ugomvi mdogo. Ata hivyo ana msamaha, haweki asira muda mrefu na hapendi lipiza kisasi.

plusnaminus

Manenoplus na minus zaidi hutumika sana katikaHisabati na mambo kama hayo ili kuwakilisha alama + (plus) na - (minus }). plus inaonyesha kuongeza, chanya nk. Minus inaonyesha kuondoa, upungufu nk.

Lakini wakati mwingine plus hutumiwa kama kiunganishi badala ya {1 kaj wakati tukiizungumzia juu ya kuongeza au kitu kama hicho. Vile minus inaweza kuchukua nafasi ya sed ne wakati si kuzungumza juu ya kuondoa au kitu kama hicho ..

 • Ĝi kostas dek eŭrojn plus kvindek cendojn. = ...kaj aldone kvindek cendojn. - Inagharimu euro 10 kujumlisha senti hamsini.=na kiujumla senti hamsini.
 • Necesas sperto plus zorgemo. = ...kaj ankaŭ zorgemo. - Inahitajika uzoefu kuongeza uangalifu.=napia uangalifu.
 • Mi pagos al vi 1000 eŭrojn minus la 100 eŭrojn, kiujn vi ŝuldas al mi. Mi do pagos sume 900 eŭrojn. - Wewe nitakulipa euro 1000 ambazo nakudai. Kwa hiyo nitawalipa jumla ya euro 900.

mara nyingineplusnaminus zinatumika kamavihusishini sawa na kun na sen, hivyo daima bila ya mwisho wa -N. Hata hivyo ni vyema kutumia kila mara plus na minus kama viunganishi kulingana na sheria kama mifano iliotajwa apo wakiweka N mwishoni wakati inahitajika.

viunganishi kati ya tumaneno .

Muda mwingine,hasa katika lugha iliyoandikwa,matumizi mamoja kaj ili kuunganisha mambo mawili au zaidi ili kufupisha sentensi.

 • Ili en- kaj el-iris tre rapide. = Ili eniris kaj eliris tre rapide. - Waliingia na kutoka kwa haraka.
 • Tio estas kombinita manĝaĵ- kaj gazet-vendejo. = ...manĝaĵvendejo kaj gazetvendejo. - Hiyo ni soko lililo changanyika kwa vyakula na magazeti.
 • Li faris multajn erarojn: skrib-, leg- kaj pens-erarojn. = ...skriberarojn, legerarojn kaj penserarojn. - Alifanya makosa mengi katika kuandika,kusoma na kufikiria.
 • Tute mankas sub-tasoj kaj -teleroj. = ...subtasoj kaj subteleroj. - Panakosekana visahani na masahani.
 • Tio estas manĝaĵ- gazet-vendejo. - Hiyo ni soko la vyakula na magazeti.
 • Tio estas manĝaĵ- sed ankaŭ gazet-vendejo. - Hiyo ni soko ya vyakula ila na magazeti pia.

Aina hizi za sentensi si za kawaida. Kwa kawaida haipendekezi, hasa wakati zina sehemu bila mwisho ambawo katika Kiesperanto kawaida hauwezekani . Ni vyema kutumia njia nyingine za kufupisha:

 • Ili iris en la domon kaj el ĝi tre rapide. - Waliingia ndani ya nyumba na kutoka nje kwa haraka.
 • Tio estas kombinita manĝaĵa kaj gazeta vendejo. - Hiyo ni soko la mkusanyiko wa vyakula na magazeti.
 • Li faris multajn erarojn skribajn, legajn kaj pensajn. - alifanya makosa mengi ya kuandika,kusoma na kufikiria.
 • Tio estas manĝaĵa gazeta vendejo. - Hiyo ni soko la vyakula au la magazeti.
 • Tio estas manĝaĵa sed ankaŭ gazeta vendejo. - Hiyo ni soko la vyakula na pia na la magazeti.
Kurudi juu