Kwa maudhui

Maneno ya kiasi wakati mwingine yako kwa namna fulani. Maneno yenye maaa ya kiasi yanaweza kuwa na nomino (multo, kelko n.k), vivumishi (multa, plurajn.k), vielezi ({1 }multe, sufiĉe n.k.), na maneno yaliyotumiwa kama vielezi (pli, tiom n.k.)

Nomino za kiasi

Nomino za kiasi ziko kama nomino za kawaida. Mara nyingi huelezewa na msemo pamoja na da ambao unaonyesha kiasi cha nini:

 • Kiam mi ien veturas, mi neniam prenas kun mi multon da pakaĵo. - Ninapokuwa na safari, sijawahi kuchukua mizigo mingi.

Kisarufi, neno la kiasi ni neno kuu, lakini kutoka kwa mtazamo neno da mara nyingi ni muhimu zaidi. Wakati mwingine, unachukulia jina la msemo na da kama vile linatambuliwa kama neno kuu:

 • Tiam grandega multo da vortoj fariĝus en la skribado tute nediferencigeblaj unu de alia. - Kisha kiasi kikubwa cha maneno kitakuwa muandiko haizekani kuyatofautisha moja kwa jingine.

  Kisarufi yasiyobadilishwa yahusiana na multo, lakini ina mwisho J, kwa sababu inahusiana na maneno kulingana na mazingira. Kwa kweli, sentensi ingekuwa ya ajabu sana, ikiwa mtu atasema yasiyobadilishwa bila J, kwa sababu maneno ya baadaye unu de alia inatia maoni ya watu kadhaa. Linganisha mfano ulfuatao: Grandega multo da vortoj fariĝas tute senbezona por lernado. (Maneno mengi sana yanakuwa hayana maana kwa kusoma)

Badala ya multo na malmulto mara nyingi wanapendelea mifumo ya vielezi multe na malmulte.

vielezi vya kiasi

Vielezi vya kiasi mara nyingi huonekana katika sentensi kama nomino yenye jukumu la kiima, shamrisho n.k. Katika matumizi ni karibu multe, sufiĉe, kelke na mabadiliko yao. Matumizi kama hayo ya kelke kwa sasa ni machache sana:

 • En la kelo troviĝas multe da rubaĵoj. - Huko jela kuna takataka nyingi.

  Multe (nyingi ya) ni kiima. Mtu anaweza pia kusema multo da rubaĵoj. (takataka nyingi)

 • El ŝia buŝo eliris kelke da perloj kaj kelke da diamantoj. - Kinywani mwake kilitoka lulu chache na almasi chache.

  Izo kelke mbili ni viima cha eliris. Mtu anaweza kusema kelko da perloj/diamantoj, lakini kelko haitumiki kamwe. Kwa sasa, wengi wanatumia kelkaj: kelkaj perloj, kelkaj diamantoj

 • La riĉulo havas multe da mono. - Tajiri ana fedha nyingi.

  Multe ni shamrisho, lakini haiwezi kuchukua mwisho N kwa sababu ni kielezi.

 • Mi havas sufiĉe da laboro. - Nina kazi ya kutosha.

Vilevile unaweza kutumia chembe za vielezi vya kiasi.

 • Ĉu vi scias, kiom estis da mortigitoj? - Unafahamu wangapi waliuwawa?

  Kiom ni kiima cha estis.

 • Prenu tiom da mono, kiom vi volas. - Chukua kiwango cha pesa unachokipenda.

  Tiom na kiom ni shamrisho.

 • Pri tiom da feliĉo mi eĉ ne sonĝis, kiam mi estis ankoraŭ la malbela anasido! - Kuhusu furaha ya kiasi hivo sikufikiria, wakati nilikuwa bado niko mtoto wa bata mchafu!

  Tiom ni adjuct pri.

 • Restas ankoraŭ iom da problemoj. - .Bado kuna matatizo fulani.

  Iom ni kiima.

 • Observu pli da ordo! - Tazama sana oda!

  Pli ni shamrisho.

 • Tro da kuiristoj kaĉon difektas. - Wapishi wengi wanaharibu mchuzi.

  Tro ni kiima.

Wakati kielezi cha kiasi kina da baada yake, inaweza mara nyingi kuonekana kwamba kiima sio neno kuu (neno la msingi kabisa). Katika upande wa maana, neno da ni neno kuu. Kwenye upande wa maana, neno da ni muhimu sana, ila kwa upande wa sarufi kielezi ni neno kuu. Ila kielezi cha kiasi + neno da ina maelezo, kawaida unahusisha maelezo hayo na neno da hata kama ni neno kuu, ingawa sio neno kuu: Multe da akvo estis verŝita sur ĝin. Lakini ikiwa neno da halipo, maelezo yanaweza kuhusishwa na kielezi tu, na kwa hiyo unapaswa kutumia fomu E: Multe estis farite.

Vivumishi vya kiasi badala ya vielezi vya kiasi.

Mara nyingi unaweza kutumia kielezi cha kiasi badala kivumishi cha kiasi. Kisha nomino ya neno da inageuka kuwa neno kuu nada hutoweka:

 • En la subtegmento troviĝas multaj malnovaj vestaĵoj....multe/multo da malnovaj vestaĵoj. - Kwenye dari kuna nguo nyingi za zamani. ≈ ...multe/multo da malnovaj vestaĵoj. (...nguo nyingi za zamani)
 • La riĉulo havas multan monon....multe/multo da mono. - Mtu tajiri ana fedha nyingi. ≈ ...multe/multo da mono.

Kuna hata hivyo tofauti. Multaj na kelkaj hutumiwa hapa juu ya masuala ya kibinafsi, ya mtu binafsi, juu ya mkusanyiko wa umati. Multe na kelke zinatumika tu kwa umati usiotofautishwa. Haikuweza kusema: Kelke da homoj sentas sin la plej feliĉaj, kiam ili vidas la suferojn de siaj najbaroj. Oni devas diri Kelkaj homoj..., kwa sababu ni hisia za kila mtu peke yake/kivyake.

Ngazi na kiasi

Ngazi na kiasi ni tofauti kabisa, lakini wakati mwingine binaonekana sawa.

Tre na multe

 • tre = "kwa ngazi ya juu, kwa uwezo mkubwa"
 • multe = "kwa kiasi kikubwa, cha muda mrefu, mara nyingi hujirudia"

Kwa vivumishi na vielezi karibu siku zote unatumia tre, ila unaweza kutumia multe, wakati kuna uwazi kwamba ni kiasi au marudio, lakini unaweza kutumia tre ikiwa ni ngazi au uwezo:

 • Ĝi estas tre bona. - Ni nzuri sana.
 • Tie troviĝas tre grandaj domoj. - Kule kuna manyumba makubwa sana.
 • Mi tre ŝatas Berlinon. = Mi intense ŝatas Berlinon. - Napenda sana Berlin. = Napenda Berline kwa kiwango cha juu.
 • Mi tre amas ŝin. = Mi intense amas ŝin. - Nampenda sana.= Nampenda tena sana
 • Mi havas multe da mono. - Nina fedha nyingi sana.
 • Ŝi multe pensis pri tio. = Ŝi longe pensis pri tio. - Alifikria sana kuhusu ile.= Alifikiria sana kuhusu ile kwa muda mrefu.
 • Kiu multe parolas, ne multe faras. - Yeyote husema mengi, hafanyi mengi.
 • Li tre multe helpis al mi. - Alinisaidia sana.

  Tre inaeleza multe. Multe inaeleza helpis.

Ili kueleza pli na tro tunatumia multe:

 • Ĝi estis multe pli granda ol antaŭe. - Ilikuwa kubwa zaidi kuliko kabla.
 • Ĝi fariĝis multe tro nigra. - Imekua nyeusi sana.

Kiel na tiel

Correlative kiel na tiel hazionyeshi namna tu, bali ngazi/kiwango pia. Yatumie katika maeneo sawa ambapo unaweza kutumia tre:

 • Vi estas tiel bela, tiel bona kaj tiel honesta, ke mi devas fari al vi donacon. - Wewe ni mzuri, ni mwema na mwaminifu kwamba ni lazima nikupe zawadi.

  Mtu anaweza kusema: mzuri sana, mwema sana na waaminifu sana .

 • La nokto estis tiel malluma, ke ni nenion povis vidi eĉ antaŭ nia nazo. - Usiku ulikuwa giza sana kwamba hatukuweza kuona chochote hata mbele ya pua zetu.

  Inawezekana kusema: giza sana.

Kiom na tiom

Correlative kiom kaj tiom huonyesha kiasi. Yanatumiwa pale ambapo unaweza kutumia multe :

 • Mi volas tiom da terpomoj, kiom mi povas porti. - Nahitaji viazi vingi ambavyo ninavyoweza kubeba.

  Unaweza kusema: volas multe na povas porti multe.

 • Ŝi tiom laboris, ke ŝi fariĝis ĉefo de la firmao. - Alifanyakazi nyingi hadi akaa bosi wa kiwanda.

  Unaweza kusema:multe laboris.

Kabla ya multe mara nyingi tunapendelea tiom, kwa sababu multe ni neno la kiasi: Nun li estis ja riĉa, havante tiom multe da mono. Au ... havante tiel multe da mono. { 2} Au ... havante tiom da mono.

"Tabia ya Tiom-kiom "

Wakati mwingine, kiom Kiom na tiom hutumiwa ikiwa ni ngazi badala ya kiel na tiel, wakati mtu anataka kusisitiza sana . Hii ni sawa kabisa. Lakini baadhi ya Waesperantiste hutumia kiom na tiom badala ya kiel na tiel kuonyesha ngazi au kiwango kama vile wanaendelea kusisitiza, kwa mfano: Mi estas tiom forta, kiom vi. Linganisha na sentensi ya msingi Mi estas tiel forta, kiel vi.Tabia hii ya " tiom-kiom -ism "ni ya kigeni kabisa kwa msingi na matumizi ya Zamenhof. Mbali na hayo, watu ambao hutumia tiom-kiom hupoteza uwezo wa kutumia tiom na kiom kwa msisitizo.

Kurudi juu