Kwa maudhui

Katika Kiesperanto kuna chembe 45 zinazoitwa correlatives kwa sababu zinaweza kupangwa katika correlatives kulingana na fomu na maana kama hiyo.

Inawezekana kusema kwamba kila correlative ina sehemu mbili, ya mwanzo na mwisho, lakini hizi correlatives kama maneno yaliokusanywa. Vipande vya correlatives huunda mfumo tofauti, uliofungwa, na haipaswi kuzichanga na vipengele vya kawaida vya lugha.

Mwanzo

KI-
maneno ya kuuliza, maneno yakuhusisha, maneno ya kulia
TI-
maneno ya kuonyesha
I-
neno lisilofasiliwa
ĈI-
Neno lote la ujumla
NENI-
Maneno ya ukanushi

Sehemu za kufuata

-U
mtu binafsi, kitu cha kibinafsi, suala la mtu binafsi
-O
kitu
-A
ubora,aina
-ES
milki, mmiliki (shamrisho, kiima)
-E
sehemu
-AM
wakati, mara (tukio, hali)
-AL
sababu
-EL
namna,kiwango
-OM
Kiasi (kiwango cha msisitizo)

Miongoni mwa mwisho wa neno correlatives ni sawa na mwisho wa kawaida, lakini maana si sawa:

KI-maneno

Maneno na KI hutumiwa hasa kama maswali na kama maneno ya kuhusiana , lakini pia kama mshangao:

  • Kio estas tio? - Kile ni kinini?/ Ile ni nini?/

    Kiulizikio.

  • Kiu kuraĝas rajdi sur leono? - nani aliye kuambia kutereza juu ya simba?

    Kiulizikiu

  • Kiel vi fartas? - Haujambo? Ukoje?

    Kiulizikiel

  • Fremdulo, diru, kiu kaj el kie vi estas. - Mgeni, sema wewe ni nani na wapi umetoka.

    Kiulizikiunakie.

  • La fera bastono, kiu kuŝis en la forno, estas nun brule varmega. - Fimbo ya chuma, iliyoko katika tanuru, sasa inawaka moto.

    kiwalilishi kiu.

  • Kiam mi venis al li, li dormis. - Wakati nilipokuja kwake alikuwa amelala.

    Kiwakilishikiam.

  • Li estas tiu, kies monon vi prenis. - Ni yule ambaye ulichukua fedha yake.

    Kiwakilishikies

  • Kia granda brulo! - Moto mkubwa kama nini!

    Mshangaokia.

  • Fi, kiel abomene! - Kwa aibu, ni machukizo gani!

    Mshangaokiel.

  • Kion mi vidas! - Ninaona nini!

    Kushangaza (na kuhojiwa) kio .

chembe chembeajn

Kielezi ajn linaonyesha kwa kurudilia usiojulikana au kutokujali. Ajn hutumiwa hasa pamoja na maneno ya KI yanayohusiana, lakini pia kwa maneno ya I na maneno ya ĈI, wakati mwingine na maneno ya NENI. Ajn daima anasimama baada ya correlative husika:

  • Mi kondukos vin al ŝi, kie ajn ŝi estos trovebla! - Nitawabeba kwake, kila mahali atakapopatikana!

    Hakuna tatizo anapopatiakana.

  • Kiu ajn ŝi estos, mi deziras al ŝi feliĉon! - Yeyote anaweza kuwa, namtakia furaha!

    Haijalishi atakuwa nani.

  • Mi donis solenan promeson, ke mi silentos, ĝis mi revenos, kiam ajn tio ĉi fariĝos. - Nilitowa ahadi rasmi kwamba nitanyamaza hadi nitakaporudi, wakati wowote itafanyika.
  • Ĉiam ajn vi estas bonvena ĉe mi. - Unakaribishwa kwangu wakati wote.

    Njoo wakati unahitaji.

  • Kial ŝi forlasis tiun lokon, en kiu ŝi havis ian ajn eblon, por ion ajn laborenspezi? - Kwa nini aliondoka mahali hapo ambako alikuwa na aina fulani ya uwezekano wa kapato mapato kikazi?

    Bila sehemu hii, uwezekano hauwezi kabisa.

  • Nenion ajn mi diros. - Sitasema chochote.

    Kabisa hakuna kitu chochote.

Kabla ya ajn Zamenhof, kwa sababu ya luga za kitaifa de naciaj lingvoj, kuna mara alitumia maneno ya KI panapohitajika ĈI au I. Ikiwa si mwanzo wa kishazi tegemezi, neno la ĈI au I inatumiwa. Mi konsentas akcepti kian ajn pagon. (Nakubali kupokea kian ajn gharama yote ile.) Vizuri zaidi: ...ĉian ajn pagon au ...ian ajn pagon.

Maneno na TI

Correlative na TI ni vionyeshi. Mara nyingi huonyesha kitu kilichotajwa hapo awali au kitu kinachotajwa muda mfupi. Vinaweza pia kuelezea kitu kinachoonekana moja kwa moja, kusikia, au mambo kama hayo:

  • Mi volas, ke tio, kion mi diris, estu vera. - Nahitaji kwamba kile nilichosema kiwe kweli.

    Tio inaonyesha jambo lililosemwa hapo awali.

  • Tio estas mia hejmo. - Hapa ndipo nyumbani kwangu.

    Tio inaonyesha kitu kinachoonekana (labda kwa kunyesha kwa kidole).

  • Li estas tiel dika, ke li ne povas trairi tra nia mallarĝa pordo. - Yeye ni mnene kiasi kwamba hawezi kupitia mlango wetu mwembamba.

    Tiel inaonyesha sentensi inayofuata ambayo ina ke.

  • Kio estas, kio vin tiel afliktas? - Je! Ni nini kinachokusumbua?

    Tielhuonyesha vitu ulivyoona au husikia.

  • Ŝi estis en tiu momento tre bela. - Alikuwa,katika muda huu,ni vizuri sana.

    Tiu inaonyesha muda uliotajwa hapo awali.

  • Tiu ĉi malfreŝa pano estas malmola, kiel ŝtono. - Mkate huu uliokauka ni ngumu kama mwamba.

    Tiu inaonyesha kitu kilichopo.

Kaneno11.4.1ĉi

Kwa correlative na TI unaweza ukaongeza neno ĉi, ili kuonyesha ukaribu na msemaji. Ĉi inaweza ikatangulia au kukaa baada ya correlative. Ĉi haiwezi kupokea mwisho. Neno la kawaida TI linaonyesha kila mara kitu kisicho karibu na msemaji. Neno na TI + ĉi linaonyesha kitu ambacho kipo karibu na msemaji:

  • tie = Katika sehemu ile → tie ĉi, ĉi tie = Katika sehemu hii karibu yangu
  • tiu domo (mbali na mimi) → tiu ĉi domo, ĉi tiu domo (karibu yangu mimi)
  • tio = kile kitu(mbali nami) → tio ĉi, ĉi tio = jambo hili
  • tiel = kwa namna hiyo → tiel ĉi, ĉi tiel = Kwa namna hii(ambavyo naonyesha)

Ĉi tiamtiam ĉi hazitumiwi katika maongezi. Badala yake neno nun (sasa) linatumiwa.

Ĉi ni neno tofauti. Usitumie kistariungio. Usiandike: ĉi-tiu, tiu-ĉi, ĉi-tie, tie-ĉi, ĉio-ĉi nk Andika: ĉi tiu, tiu ĉi, ĉi tie, tie ĉi, ĉio ĉi nk.

Lakini mara nyingi tunaunda kivumishi au vielezi kutoka kwenye kipengele cha sentensi ambacho kina chembe ĉi. Muda huo maneno yote huwa neno moja . Kwa kawaida neno la TI hupotea. Kwa usahihi basi ni desturi kuweka kistariungio baada ya ĉi: ĉi tieĉi-tiea, en tiu ĉi noktoĉi-nokte, sur ĉi tiu flankoĉi-flanke, la somero de tiu ĉi jarola ĉi-jara somero.

maneno na I

Correlative na I huwakilisha mambo yasiyotajwa au yasiyojulikana:

  • Ŝi ricevis ion por manĝi kaj por trinki. - Alipata vitu vya kula na kunywa.

    Haikutajwa nini alipokea.

  • Venis iuj personoj, kiujn mi ne konas. - wapo watu walikuja ambao sikuwafahamu.

    Hatujuwi walikuwa watu gani..

  • Ili iam revenos. - Iakati mwingine watarudi. (Ipo siku watarudi)

    Hatua kwa wakati haijulikani.

  • Hodiaŭ estas ies tago de naskiĝo. - leo ni sherehe ya kuzaliwa kwa mtu fulani.

    Haijatajwa ni nani mwenye siku ya kuzaliwa.

maneno na N

Correlative na ĈI huonyesha kitu chochote:

  • Li faris ĉion per la dek fingroj de siaj manoj. - Alifanya kila kitu kwa vidole kumi vya mikono yake.

    Ĉio inaonyesha vitu vyote ambavyo alifanya.

  • Ĉiu homo amas sin mem. - kila mtu anajimpenda mwenyewe.

    Hakuna mtu aliyepo ambayo hii haifai.

  • Tiuj ĉi du amikoj promenas ĉiam duope. - Marafiki hawa wawili daima wanatembea pamoja. (duope - katika jozi nk)

    Ĉiam (daima) huonyesha kuwa hakuna wakati ambao hawaendi pamoja.

  • Ĉie regis ĝojo. - Pote palikuwa furaha.

    Hapakuwa na sehemu ambapo hapakuwa furaha.

Wakati mwingine chembe ĉi hutumiwa kabla au baada ya correlative ya ĈI: ĉio = hivi vitu vyote → ĉio ĉi, ĉi ĉio = mambo haya yote, yote hapa.

Maneno na NENI

Correlatives za NENI zina maana ya ukanushi:

  • La tempon venontan neniu ankoraŭ konas. - Muda wa kuja hakuna aujuae.

    Neniu inamaanisha kwamba hakuna mtu yeyote ambaye anajua muda ujao.

  • Mi neniel povas kompreni, kion vi parolas. - Hkuna namna naweza kuelewa nini unachokisema.

    Neniel inaonyesha kwamba kwa namna yoyote siwezi kukuelewa.

  • Kiam mi ien veturas, mi neniam prenas kun mi multon da pakaĵo. - Wakati nasafiri sehemu mimi kamwe sichukui mizigo mingi.

    Neniam inaonyesha kwamba hakuna wakati ambapo mimi nachukua mizigo mingi kwenye safari.

neno na NENI hutosha kukanusha sentensi nzima .

Correlative na U

kiu
Huuliza kuhusu utambulisho wa mtu mmoja kati ya watu wengi wanaojulikana, vitu au mambo.
tiu
Huonyesha mtu anaejulikana kati ya watu wengi, vitu au mambo.
iu
Huonyesha mtu asiyejulikana au asiyefahamika, kitu au jambo.
ĉiu
Inaonyesha mtu/kitu kimoja na bila kusahau watu wa kikundi cha watu, kitu au mambo.
neniu
Inakanusha watu wa kundi la watu, vitu au mambo.

Maneno na U yanaonyesha kibinafsi na utambulisho. Ni maneno ya msingi zaidi kwenye correlative.

Correlatives na U zinaweza kupokea mwisho N na J. Pamoja na mwisho J, zinaonyesha watu kadhaa, vitu, au mambo kadhaa.

Correlative na U ni fafanuzi. Kwa hiyo, la inaweza kuachwa kutumia.

Correlative na U ni wasifu wa nomino, lakini nomino hiyo mara nyingi hainaeleweki. Ikiwa hakuna kitu katika mazingira kinachoonyesha vinginevyo, ni tunadhani kwamba ni neno "persono (j) (n)" (mtu / watu):

  • Kiu libro estas via?Kiu estas via? - Ni kitabu kipi cha kwako?→Chako ni kipi?
  • Tiu seĝo ŝajnas bona.Tiu ŝajnas bona. - Kile kiti kinaonekana kuwa ni kizuri.→ kile kinaonekana ni kizuri.
  • Ĉiu homo devas pensi mem.Ĉiu devas pensi mem. - Kila mtu lazima afikirie.→Kila mmoja hufikiria.
  • Kiu persono venis?Kiu venis? - Mtu yupi aliekuja?→ Yupi aliekuja?
  • Ĉu estas iu [persono] en la kuirejo? — Jes, Paŭlo estas tie. - Kuna mtu yeyote jikoni?- Ndiyo,Paulo yuko kule.
  • Jen kelkaj bonaj libroj. Kiun [libron] vi volas legi? — Mi volas tiun [libron]. - Kuna miongoni mwa vitabu vizuri hapa.Kipi[kitabu]unahitaji kusoma?-Nahitaji hiki.
  • Ĉu vi havas krajonon? — Neniun [krajonon] mi havas. - Unakalamu ya mkaa? -Sina ata moja.

Ĉiu(j) daima liko mu wingi, lakini utofauti hutolewa kati ya umoja ĉiu (kila) na wingi ĉiuj (yote/wote).

  • Neno ĉiu linatumika wakati wa kuzingatia watu binafsi.
  • Ĉiuj hutumiwa wakati wa kufikiri juu ya kundi zima kuchukuliwa pamoja.

Wakati mwingine tofauti hii si muhimu, lakini katika hali nyingine, tofauti ni kubwa:

  • Por ĉiu tago mi ricevas kvin eŭrojn. = Por ĉiu aparta tago... - Kila siku ninapata euro tano. = Kwa kila siku moja ...
  • Ĉiu amas ordinare personon, kiu estas simila al li. = Ĉiu aparta homo amas... - Kila mtu humpenda mtu ambaye ni anafanana naye mwenyewe. = Kila mtu binafsi anapenda ...
  • Kvinope ili sin ĵetis sur min, sed mi venkis ĉiujn kvin atakantojn. = ...mi venkis la tutan grupon. - Watano miongoni mwao walijirusha juu yangu, lakini nikawashinda washambuliaji wote watano. = Nimepiga kundi zima.

    Hapa J ni muhimu kwa sababu nambari ya tano imetajwa. Lakini kwa njia nyingine unaweza kusema: ...mi venkis ĉiun el la kvin atakantoj. Lakini hapo hatuzungumzii pambano dhidi ya kundi lote bali mapambano matano tofauti .

  • Post la kurado ĉiuj estis terure lacaj. - Baada ya kukimbia,wote walikuwa katika hali ya kuchoka.

    Tunazungumzia kuhusu kundi zima la wakimbiaji. Mtu anaweza pia kusema: ... Wote walikuwa wamechoka sana. (kila mmoja alikuwa amechoka sana)

  • El ĉiuj miaj infanoj Ernesto estas la plej juna. = El la tuta grupo de miaj infanoj... - Kati ya watoto wangu wote Ernesto ni mdogo zaidi. = Kati ya kundi zima la watoto wangu ...
  • Nun mi legas, vi legas kaj li legas; ni ĉiuj legas. - Kwa sasa ninasoma,unasoma na yeye anasoma; Sisi sote tunasoma.

    Ni ni wingi. Kwa hiyo ĉiuj lazima awe na J.

Neniu ya kujitegemea ni kawaida kuonekana peke yake bila mwisho J:

  • La tempon venontan neniu ankoraŭ konas. Neniu = neniu persono. - Wakati ujao hakuna mtu anayejua. Neniu (hakuna mtu) = hakuna mtu.
  • Mi konas neniun en tiu ĉi urbo. - Simfahamu mtu yeyote katika mji huu.

Neniu,Bila ya nomino yakufuta unatumia neniu bila J:

  • Ŝi ne vidis eĉ la ĉielon, ĉar ĝi estis kovrita de nuboj kaj neniu stelo en ĝi brilis. - Yeye hakuweza na hata kuona anga, kwa sababu ilikuwa imefunikwa na mawingu na hakuna nyota hata moja ilikuwa inaangaza (ndani yake).

Hata hivyo unaweza kutumia neniuj kuonyesha utofauti wa wazo "zaidi ya moja", lakini kawaida hufanyika tu wakati linafuatiwa na nomino:

  • Ĉe la fenestro restis plu neniuj floroj. - Dirishani pale hakuna hata masalio ya maua.

    Mwanzo palikuwa maua mengi.

Correlative na O

kio
''Jambo gani, aina gani ya jambo''
tio
''jambo lile''
io
''kitu kimoja, aina ya kitu''
ĉio
"kila jambo, kila aina ya suala"
nenio
''hakuna jambo,hakuna aina ya jambo''

Correlatives na O zinaonyesha kitu, au suala ambalo haliwezi kuitwa kwa nomino. Hapa neno "jambo" linatumiwa kama maelezo, lakini maana ni zaidi ya jumla. Correlatives na O zinatumiwa pia kuwakilisha kitu ambacho kinaelezwa kwa sentensi nzima.

Correlative na O zinaweza kuchukua mwisho N, lakini kwa kawaida hazichukuwi mwisho J, kwa sababu yanaelezea vyote jumla.

Wasifu wa correlatives na O husimama kila mara baada ya correlative: io bona, kion novan, ĉio grava n.k.

Correlatives na O ni ni maneno yanayojitegemea. Hayawezi kuelezea nomino. Wanajibu neno la U + :

  • Kio estas tio? = Kiu afero estas tiu afero? - Kile ni nini?=Ni kitu gani hiki ni kitu?
  • Tio estas speco de meblo. = Tiu afero estas speco de meblo. - Hiyo ni aina ya fanicha. Jambo hili ni aina ya fanicha.
  • Ĉio restis kiel antaŭe. = Ĉiu afero restis kiel antaŭe. - Kila kitu kilibaki kama mwanzo .=Kila jambo lilibaki kama mwanzo.
  • Kion bonan vi trovis tie? = Kiujn bonajn aferojn vi trovis tie? - Ni kipi kizuri ulipata kule?=Ni vitu vipi vizuri/mambo ulioyo pata kule?
  • Nenion interesan mi trovis. = Neniun interesan aferon mi trovis. - Sikupata kitu cha kuvutia. = Sijaona jambo la kuvutia.

Wakati mwingine mtu anaweza kusita kati ya tio na ĝi. Kwa kawaida tunatumia tio kwa kitu kisichojulikana ambacho hatuwezi au hatutaki kutaja kwa jina wazi.Unapaswa kutumia tio ili unyeshe kitu ambacho kinatajwa kwa sentensi nzima. Tunatumia ĝi kwa kitu kilichofafanuliwa ambacho kimeonyeshwa kwa nomino hapo awali na kunaweza kurudia kwa nomino hiyo hiyo pamoja na la au wasifu nyingine:

  • Ŝi rakontis belan fabelon. Tio estis tre amuza. - Aliiambia hadithi nzuri. Hiyo ilikuwa ya kufurahisha sana.

    Cha kufurahisha ni kuniambia hadithi. Tio inawakilisha sentensi nzima ya awali.

  • Ŝi rakontis belan fabelon. Ĝi estis tre amuza. - Aliiambia hadithi nzuri.Hiyo ilikuwa ya kufurahisha sana.

    Ilikuwa ni hadithi ambayo ilikuwa ya kusisimua. Ĝi inawakilisha kipengele cha sentensi la (bela) fabelo.

Correlative na A

kia
''aina ipi,ina ubora upi''
tia
"wa aina hiyo, ikiwa na ubora huo"
ia
''ya aina fulani, ikiwa na aina fulani''
ĉia
"ya kila aina, ikiwa na ubora wote"
nenia
"bila aina yoyote, isiyo na ubora wowote"

Correlatives na A zinatumika kama vivumishi. Zinachukua mwisho J na N kama sheria za vivumishi. Ila correlative na A zinaonyesha kila mara ubora na aina kipindi vivumishi halisi (vyenye mwisho A halisi) vinaweza kuwa na maana nyingi.

Correlatives na A ni wasifu. Kwa hivyo mtu hawezi kutumia la nazenyewe.

  • Kia li estas? Ĉu li estas maljuna aŭ juna? - Yuko vipi? Je! Yeye ni mzee au kijana?
  • Kian aĝon vi havas? - Wewe una umri gani? (una umri wa aina gani)
  • Kia estas via nomo? - Unaitwa nani? Jina lako nani?

    Au: Kiu [el ĉiuj nomoj] estas via nomo? Au mara nyingi zaidi: Kio estas via nomo? Zamenhof alitumia pia: Kiel estas via nomo? Hata hivyo tunasema mara nyingi: Kiel vi nomiĝas?

  • Be! li staris senhelpe, tian respondon li ne atendis. - Huh! Yeye alisimama pale bila msaada, aina hiyo ya jibu yeye hakutarajia.
  • Estis tia ventego, ke la tegoloj deflugis de la tegmentoj. - Palikuwa upepo mkali mpaka matofali yalitoka juu yakaruka.
  • Restu ĉiam tia, kia vi estas! - Kila siku uishi kama ulivyo!

    Tia inaelezea sentensi ya kia inayofuata. Ikiwa baada ya tia hakuna sentensi nzima (pamoja na prediketo), lakini tu kifungu, basi hatutumii kia, lakini yakulinganisha kiel{ 2}: Li estas tia kiel mi. (Yuko kama mimi)

  • Mi ne volis trinki la vinon, ĉar ĝi enhavis en si ian suspektan malklaraĵon. - Sikuhitaji kunywa divai kwa sababu ilikuwa na kitu cha kutia mashaka.
  • Maldiligenteco estas la radiko de ĉia malbono. - Uvivu ni mzizi a uovu wote.
  • Nenia konstruo povas esti sen bruo. - Hakuna ujenzi bila kuwa na kelele.

Correlatives na A zinaonyesha ubora na aina wakati correlativa na U inaonyesha utambulisho. Kwa kia/kiu na tia/tiu tofauti kawaida iko wazi. Kwa ia/iu, ĉia/ĉiu na nenia/neniu kuna utofauti mdogo:

  • Kia homo li estas? - Ni mtu wa aina gani?

    Wanata tabia za mtu.

  • Kiu homo li estas? - Ni mtu yupi?

    Tuna uliza,kwa mfano, kuhusu jina la mtu ili wajuwe utambulisho wake.

  • Tia opinio estas tute erara. - Aina hiyo ya maoni ni si sahihi.

    Maoni yote ya aina hiyo si sahihi

  • Tiu opinio estas tute erara. - Maoni haya niya makosa kabisa.

    Maoni yaliyojadiliwa ni ya makosa. Maoni mengine yanayofanana labda ni sahihi.

  • Ni devas enloĝiĝi en ia hotelo. = ...en hotelo de iu el la diversaj specoj de hoteloj. - Tunapaswa kuangalia katika aina fulani ya hoteli. = kati ya moja ya aina tofauti za hoteli.
  • Ni devas enloĝiĝi en iu hotelo. = ...en iu el la diversaj individuaj hoteloj, kiuj troviĝas ĉi tie. - Tunapaswa kuangalia katika hoteli fulani. = kati ya mojawapo ya hoteli kadhaa zinazopatikana hapa.

    Kawaida tunatoa iu kwa aina hii ya sentensi.

Correlative na ES

kies
"ya nani"
ties
"ya mtu yule"
ies
ya mtu fulani
ĉies
ya kila mtu
nenies
"sio ya mtu, hakuna hata mmoja"

Neno - ES, ambalo ni wasifu wa nomino, linaongeza maana inayoelezeka. Maneno na ES ni wasifu - kama vile viwakilishi milikishi - hivyo hatuwezi kutumia la pamoja na hayo. Ikiwa tunachukua nafasi ya neno la ES kwa ktumia de, tunapaswa kuongeza la.

Kama viwakilishi vimilikishi neno la ES husimama kabla ya nomino, wakati na mwenzake de huja baada:ties libro=la libro de tiu (mtu). (kitabu cha huyu)

Neno na ES halichukui mwisho J wala mwisho N

  • Kies filino vi estas? - Wewe ni binti wa nani?
  • Mi efektive ne scias, kies kulpo ĝi estas. - Mimi, kwa kweli, sijui ni kosa la nani.
  • Ili ekvidis virinon, kies vizaĝon ili en la krepusko ne rekonis. - Walimuona mwanamke ambaye uso wake hawakujulikanaa wakati wa kisikusiku.
  • Kies gasto mi estas, ties feston mi festas. - Mimi ni mgeni wa nani, sikukuu ya mtu huyo nahudhuria.

    Ties hayatumiwi mara nyingi. Tunapendelea kutumia viwakilishi vimilikishi (lia, ŝia, ĝia au ilia).

  • La infano ludis kun sia pupo, kiam subite ties kapo frakasiĝis. - Mtoto alikuwa akicheza na mdolo wake wakati ghafla kilikatika kichwa chake.

    Ties huonyesha kwamba tunazungumzia kuhusu kichwa cha mdoli. Ikiwa ni kichwa cha mtoto, mtu angeweza kusema ĝia kapo. (kichwa chake)

  • Kiu ĝojas pri ies malfeliĉo, tiu ne restos sen puno. = ...pri la malfeliĉo de iu persono... - Yeyote anayefurahia tabu ya mtu mwingine huyo hatakosa adhabu = kuhusu tabu ya mtu mwingine ...

    Ies (ya mtu, ya mtu yeyote) kawida hutumiwa kwa mtu mmoja tu asiyejulikana(hakuna vitu,wala kuhusu mambo kadkalika au watu) .

  • Tio estis la koro de riĉa fama viro, kies nomo estis sur ĉies lipoj. = ...sur la lipoj de ĉiuj personoj. - Huo ndio moyo wa mtu tajiri, maarufu, ambaye jina lake lilikuwa kwenye midomo ya kila mtu. = ... kwenye midomo ya kila mtu .

    Ĉies kawaida hutumika kwa watu, si kwa vitu.

  • Memoru, ke Esperanto estas nenies propraĵo. - Kumbuka kwamba Kiesperanto si mali ya mtu yeyote.

    Nenies (si ya mtu) kawaida hutumika tu kuhusu watu, si kuhusu vitu.

Correlative na E

kie
"Wapi,katika sehemu gani"
tie
"kule,katika ile sehemu"
ie
"sehemu fulani,katika sehemu fulani"
ĉie
"mahali popote,katika kila sehemu,katika kila sehemu"
nenie
"hakuna sehemu"

Correlative na E haiwezi kuchukuwa mwisho J, lakini unaweza kuongeza mwisho N kuonyesha mwelekeo :

kien
"kwa sehemu ipi, katika mwelekeo upi"
tien
"kwa mahali hapo, katika mwelekeo huo"
ien
"kwa sehemu fulani, kwa upande fulani"
ĉien
"kwa kila mahali, katika kila upande"
nenien
"hakuna sehemu, hakuna mwelekeo"
  • Kie estas la libro kaj la krajono? - Kitabu na penseli viko wapi?
  • Mi montris al la infano, kie kuŝas ĝia pupo. - Nilimuonyesha mtoto wapi mdoli wake amelala.
  • Sonorado al li venas, sed de kie — li ne komprenas. - Kengele ilipigwa kwake, lakini kutoka huko,-hakuweza kufahamu.
  • Mi volis resti tie, kie mi estis. - Nilihitaji kubaki kule ambapo nilikuwa.
  • Se li scius, ke mi estas tie ĉi, li tuj venus al mi. - Kama angefahamu kuwa niko hapa, angelikuja kwangu haraka.
  • Ĉu vi loĝas ie? = Ĉu vi loĝas en iu loko? - Je, unaishi mahali fulani? = Je, unaishi katika mahali fulani?
  • Malsaĝulo ĉie sian nomon skribas. - Mpumbavu huandika jina lake kila sehemu.
  • Pli bela reĝidino ol ŝi troviĝis nenie en la mondo. - Mtoto wa kifalme mzuri zaidi ni kuliko yeye hakuonekana popote duniani.
  • Kien vi iras? — Mi iras en la ĝardenon. - Unakwenda wapi? - Ninakwenda bustanini.
  • Rigardu tien ĉi. - Tazama hapa.
  • Mi nenien plu iros hodiaŭ. - Sitakwenda mahali popote leo.

Correlative na AM

kiam
"lini,ni katika muda gani, juu ya wakati upi"
tiam
"wakati huo, mara hiyo"
iam
"kwa muda fulani, mara fulani"
ĉiam
"siku zote, muda wote, kila wakati"
neniam
"kamwe, hakuna muda, hakuna fursa"

Maneno na AM hayachukui mwisho N wala N

  • Sed kiam tio okazis? - Lakini wakati gani hili lilitokea?

    Wakati wa kuuliza kuhusu wakati sahihi (muda wa saa), hatutumii kiam, lakini kiulizi cha oda kioma.

  • Li skribis al mi, ke li intencas ĝin eldoni, sed li ne skribis ankoraŭ kiam li ĝin eldonos. - Aliniandikia kwamba anapanga kukitoa , lakini tayari hakuandika lini atakitoa.
  • En unu tago, kiam ŝi estis apud tiu fonto, venis al ŝi malriĉa virino. - Siku moja wakati alipokuwa kwenye chemchemi hiyo, mwanamke maskini alikuja kwake.
  • Tubeto, en kiun oni metas cigaron, kiam oni ĝin fumas, estas cigaringo. - Kitunga kidogo ambacho wanaweka sigara wanapovuta moshi wake, ni chombo cha sigara.
  • De kiam vi loĝas ĉi tie? - Tangu lini uliishi hapa?
  • Li vekiĝis nur tiam, kiam la suno leviĝis. - Aliamka tu wakati jua limechomoka.
  • Ŝajnas al mi, ke ĉi tiun vizaĝon mi jam iam vidis. - Imeonekana kwangu kwamba tayari nimeuona uso huu wakati fulani.
  • Ŝi estis ja la plej bela knabino, kiun li iam vidis. - Alikuwa mschana mzuri zaidi ambae hajawahi kuonekana.

    Iam huwakilisha muda mwingine katika wakati uliopita.

  • Oni diras, ke la vero ĉiam venkas. - Wanasema kwamba ukweli kila mara hushinda. (lit. Ukweli utashinda daima)
  • Bona koro neniam fariĝas fiera. - Moyo mzuri haujawahi kujivuna.
  • La maljunulo fermos por ĉiam siajn okulojn. - Mzee atafunga macho yake daima.

    Msemo por ĉiam inaonyesha kuwa matokeo yatabaki daima. Kufumba macho ni kwa muda mfupi tu, lakini kile kinachofuata, macho kufungwa, itakuwa milele.

Correlative na AL

kial
"kwa nini, kwa sababu gani"
tial
"kwa hiyo,kwa sababu hii, kwasababu ya"
ial
"kwa sababu fulani, kwa sababu fulani, kwa sababu ya kitu"
ĉial
"kwa kila sababu, kwa kila sababu, kwa sababu ya kila kitu"
nenial
"hakuna sababu"

Maneno na AL hayachukui mwisho J au mwisho N.

  • Kial vi ploras? - Kwa nini unalia?
  • Mi komprenas, kial vi faris tion. - Nimefahamu kwanini unafanya hivyo.
  • Hodiaŭ estas bela frosta vetero, tial mi prenos miajn glitilojn kaj iros gliti. - Leo tuna hali ya hewa nzuri , hivyo nitawachukua vipungu vyangu niente kuteleza.

    Angalia tofauti kati ya tial (kwa hiyo, ndiyo sababu) na ĉar. Tial inawakilisha sababu, lakini ĉar(kwa sababu) inaanzia kishazi tegemezi kinachoonyesha sababu: Nitachukuwa vipungu vyangu niende kuteleza, kwa sababu kuna hali ya hewa nzuri.

  • Mi vin ial ankoraŭ ne konas. - Kwa hali fulani bado sijakufahamu.
  • Vi demandas, kial mi amas vin. Mi respondas: ĉial! - Unauliza kwa nini ninakupenda. Najibu: kwa kila sababu!

Neno nenial linatumika marachache, lakini linapotumiwa, linakanusha sentensi nzima (kama vile maneno mengine yote ya NENI):

  • Tian Regularon por nia Ligo mi nenial povus aprobi. = ...mi pro neniuj motivoj povus aprobi. - Hakuna sababu ambayo ingeniruhusu mimi kupitisha aina ya sheria hiyo kwa ligi yetu. = ... hakuna sababu ningeweza kupitisha.
  • Vi povus inciti lin kiom ajn. Li nenial kolerus. = ...li pro neniu kaŭzo kolerus. - Unaweza kumchepesha kwa kiwango chochote. Yeye hangekuwa na sababu ya kukasirika ... = ... hakuna sababu ingeweza kumkasirikia.

Ikiwa unataka kuonyesha tafsiri nzuri zaidi, tumia sen kaŭzo, senkaŭze, senmotive aŭ kama hivyo: Ŝi ridis senkaŭze. = Ŝi ja ridis, sed sen motivo.. (Alicheka bila sababu)

Correlatives na EL

kiel
"jinsi; kwa namna gani au kwa kiwango gani"
tiel
"katika namna hiyo au kwa kiwango hicho"
iel
"kwa namna fulani, kwa kiwango fulani"
ĉiel
"katika kila njia"
neniel
"hakuna njia"

Maneno na EL kwa jumla ni maneno yaanayo tumiwa kama vielezi ambayo yanatumika ikiwa haihusu wakati (maneno na AM ), mahali ( Maneno na E , sababu ( maneno na AL ) au kiasi / idadi ( maneno na OM). Maneno naa EL hufunika sana maana nyingine zote ambazo vielezi vinaweza kuonyesha. Mara nyingi inaonyesha kiwango na namna.

Maneno na EL hayachukuwi mwisho J au mwisho N.

  • Kiel li aspektas? - Anafanana aje?
  • Kiel vi fartas? - Habri gani?(unajisikia namana gani?)
  • Rakontu al mi per malmulte da vortoj, kiel tio okazis. - Niambie kwa maneno machache jinsi hii ilivyotokea.
  • Mi zorgas pri ŝi tiel, kiel mi zorgas pri mi mem. - Ninamjali kama ninavyojijali mimi mwenyewe.
  • Kiel alta estas tiu turo? - Jinsi gani mnara huo ni mrefu?
  • Kiel longe tio ankoraŭ daŭros? - Bado itachua muda wa kiasi gani?
  • Tiu ĉi malfreŝa pano estas malmola, kiel ŝtono. - Huyu mkate mkavu ni mgumu kama jiwe.
  • Bojas hundido, ĉar tiel faras la hundo. - Mbwa anabweka kwa sababu mbwa wanafanya hivyo.
  • Ne faru tiel, faru tiel ĉi! - Usiifanye kwa njia hiyo, fanya kwa njia hii!
  • Ili ambaŭ estis tiel malagrablaj kaj tiel fieraj, ke oni ne povis vivi kun ili. - Wote wawili walikuwa hawakubaliki na wakujuvuna hivyo hawakuwezi kuishi nao.
  • Mi estas tiel forta, kiel vi. - Ninanguvu kama wewe.
  • Iel ni sukcesos. - Kwa namna fulani tutafanikiwa.
  • Ili ĉiel helpis al mi. - Walinisaidia katika kila njia.
  • Mi neniel esperis sukceson. - Sikuweza kuwa na matumaini kwa namna yoyte ya kufauru.

Correlative na OM

kiom
"kiasi gani, ni idadi gani, ni kiasi gani cha"
tiom
"kiasi hicho, kiasi hicho, kiasi hicho"
iom
"siyo sana lakini pia si kidogo"
ĉiom
"kiasi kizima"
neniom
"hakuna idadi, hakuna aina ya kiasi, hakuna aina ya kipimo"

Maneno na OM hayawezi kuchukua mwisho J wala mwisho N.

  • Kiom vi volas, ĉu du aŭ tri? = Kiel multajn vi volas... - Unahitaji kiasi gani, mbili au tatu?= Unataka kiasi gani...
  • Ŝi pripensis, kiom kostos al ŝi la nokta restado. - Alizia ngapi usiku mmjo utamgharimu.
  • Ho, kiom pli bona estas via amo, ol vino! - Oh, divai, upendo wako ni mzuri kuliko nini!
  • Kiom mi vidas, vi havas nur unu filon. = Laŭ tio, kion mi vidas, vi havas... - Kwa kile ninachokiona, una kijana mmoja tu.= (Vile ninavyoona)kulingana na kile ninachoona, una ...

    Inawezekana una vijana wengi, lakini siwezi kuona zaidi.

  • Sendi 100 ekzemplerojn mi ne povis, ĉar mi nun tiom ne havas. - Sitaweza kuagiza nakala 100, kwasababu sina nazo hizo kwa sasa.
  • Mi havas tiom multe, ke mi ne bezonas ŝpari! - Ninazo nyingi hivyo sihitaji kuzihifadhi!

    Mara nyingi kiom na tiom hutumiwa pamoja na multe (aŭ multaj ). Multe inaweza kuachwa, lakini inaimarisha maana fulani. Unaweza pia kutumia kiel multe, tiel multe, lakini hakuna msisitizo.

  • Ŝi aĉetis iom da butero. = ...kvanton da butero ne tre grandan sed tamen konsiderindan. - Alinunua siagi. = si kiasi kikubwa cha siagi lakini bado ni kubwa.

    Katika nadharia iom inapaswa kumaanisha "kiasi kisichojulikana", lakini daima huonyesha kiasi kidogo. Kwa maana ni maalum kabisa, yaani: "sio nyingi sana, lakini bado ni vya kutosha kuchukuliwa kuwa muhimu, ili iwe na maana ". Usichanganye iom (kiasi fulani) na malmulte (-chache): Alifanya makosa fulani. Hakukuwa na makosa mengi sana, lakini yanatosha ili wamlaumu. Alifanya makosa machache. Makosa yalikuwa machache sana kwamba mtu anapaswa kumsifu.

  • Mi pensas, ke mi ĝin ankoraŭ iom memoras. = ...ne tre multe memoras, sed ankoraŭ ja memoras. - Nafikiri kwamba bado naikumbuka kiasi fulani.=....si sana ila bado nakumbukakidogo
  • Tie supre estingiĝis la ruĝaj koloroj, dum la suno iom post iom malaperis. - Huko juu palikuwa rangi nyekundu, wakati wa jua lilipotea kidogo kidogo.

    Msemo iom post iom unaonyesha kwamba kitu kilichotokea kwa mabadiliko mengi madogo, ambayo kidogoyasitambuliki.

  • Kiom da benzino vi volas? — Mi volas ĉiom, kiom vi havas. = ...Mi volas la tutan kvanton da benzino, kiun vi havas. - Unahitaji kiasi gani cha gesi? Nahitaji kiasi chote ambacho unacho. = ...nataka kiasi chote cha gesi ambacho unacho.

    Maana ya ĉiom katika matumizi mara inafanana na maana ĉio,ambayo hutumiwa mara nyingi.

  • Sur la mezo de la strato estas multe da radoj kaj da ĉevalaj hufoj, sed da homoj piedirantaj estas malpli, preskaŭ neniom. - Katikati ya barabara kulikuwa na magurudumu mengi na kwato za farasi, lakini kulikuwa na wachache wa miguu, karibu hakuna.

Maneno na OM hutumika kama vielezi na kama nomino.

Kawaida kwa kuonyesha kiwango tunatumia kiel na tiel. Ila kwa msisitizo mkubwa, unaweza kutumia badala yake kiom na tiom: Ĝi estis tiom bela, ke mi svenis. La Esperantistoj tute ne pretendas, ke ilia lingvo prezentas ion tiom perfektan, ke nenio pli alta jam povus ekzisti.

Maneno na ALI- yanaweza kuwa correlatives?

Mara nyingi walipendelea kuongeza kwenye correlatives neno * ALI- * wakiunda mfululizo mpya aliu, alio, alia, alies, alie, aliam, alial, aliel, aliom*. Wengine hufanya hivyo kwa kutumia hasa maneno aliel na alies

Katika Kiesperanto rasmi, ALI ni mizizi ya kawaida, ambayo inayoweza kutumika kuunda maneno kwa kutumia mwisho wa kawaida.

  • alia = "siyo sawa, tofauti"
  • alio = "kitu kingine"
  • alie = "kwa wakati mwingine,katika namna nyingine"
  • alii = "kuwa wa aina nyingine, kuwa tofauti"(hutumiwa mara chache)

Kuanzisha matumizi ya maneno correlatives yanaweza kuleta mabadiliko makubwa katika lugha. Hapa ni mifano michache tu:

Neno la kawaida alie mara nyingi linamaanisha "wakati mwingine", lakini pia linaweza kumaanisha "kwa namna nyingine". Hata hivyo, * alie * lingekuwa badala yake linamaanisha "mahali pengine". Kisha sentensi za kawaida kama Ni devas alie agi yatabadilisha maana yake.

Aliakwa hali ya kawaida katika Kiesperanto kwa kawaida sio correllative lakini kivumishi cha kawaida, na kina maana "ya aina nyingine" au "na utambulisho mwingine". Correlative mpya alia kingekuwa kinamaanisha tu "ya aina nyingine" Ikiwa pangekuwa correlative na ALI, basi mtu hawezi kusema, kwa mfano, la alia ĉambro estas pli granda, ila la aliu ĉambro estas pli granda, Ungepaswa kusema ili amas unu la aliun badala ya ili amas unu la alian.

Mara nyingi unafanya mkusanyiko wa maneno kama: de alia specoalispeca. Lakini watumiaji wa correlatives na ALI lazima badala yake waseme: aliuspeca, kwa sababu huwezi kuondoa sehemu ya mwisho ya correlatives. Linganisha na: de tiu specotiuspeca(ne: tispeca).

Hakuna ambaye alitumia maneno yote ya correlatives na ALI kwa mfululizo kwa namna inayofaa. Hadi sasa tunaona tu matumizi yasiyofaa ya aliel na alies, na mara kwa mara aliu. Wengine hutumia lugha ya Kiesperanto ya kawaida na lugha iliyobadilishwa. Wakati wanasema, kwa mfano, alie au alia, hujui kama kutafsiri kwa maana ya jadi au kulingana na lugha mpya. Kwa bahati nzuri, hata hivyo, wengine bado wanatumia lugha kwa kawaida na kwa mantiki.

Kwahiyo, tumia maneno ya correlatives yanayojulikana, na elezea mambo mengine ukitumia mizizi ya kawaida kulingana na sheria ya msingi ya Kiesperanto .

Mageuzi yanayoonekana Kiesperanto rasmi
aliu alia
alia alia, alispeca, alieca
alies de alia (persono), aliula
alie aliloke
alien aliloken
aliam alifoje, aliokaze
alial alikaŭze
aliel alimaniere, alie
aliom alikvante

Angalia: Kama "maelewano" kulikuwa na pendekezo ya fomu aliio, aliiu, aliia, aliie }, aliiel nk (mkusanyiko wa mzizi ALI na correlatives na I). Ingawa maneno haya ni ya kawaida hawapaswi kabisa katika matumizi ya vitendo. Si rahisi kusikia tofauti kati ya aliie na alie, kati ya aliia na alia, nk . Haitoshi maneno hayo yanaunganishwa mara kwa mara. Yanapaswa pia kutumika katika mawasiliano.

Kurudi juu