Kwa maudhui

Ne

Kukanusha tunatumia maneno ne. Ne linakanusha neno ambalo liko baada yake. Kwa kawaida ne husimama kabla ya prediketo, na wakati unakanusha prediketo unakanusha sentensi nzima.

 • Mi ne dormas. - silali

  sio hivyo, ninavyolala. Kulala kwangu kumekataliwa.

 • Al leono ne donu la manon. - usimpe simba mkono.
 • La patro ne legas libron, sed li skribas leteron. - baba hasomi kitabu, ila anaandika barua.

  Kukanusha kunahusisha kitenzi legas. Kitenzi skribas na kila kinachoambatana kinaendelea kuwa halali.

Ukanushaji kwenye kishazi tegemezi hutumika ndani ya kishazi tegemezi tu: Mi diris, ke mi ne venos. (nilisema kuwa sitakuja) Ukanushaji unaathiri prediketo ya kishazi tegemezi tu venos. Sentensi nzima ni kinishi: Nilisema hivyo.

Wakati mwingine hutokea kwamba prediketo iliokanushwa haieleweki vizuri: Ĉiu povu vidi, kiu el la vastigantoj plenumas sian promeson kaj kiu ne. ukanushaji unaathiri kitenzi ambacho hakieleweki vizuri plenumas: ...kaj kiu ne plenumas sian promeson.

Ne pia ni neno la jibu.

Correlative na NENI

Kwa kukataa unaweza pia kutumia correlative na NENI. Neno NENI- hutosha kwa kukataa prediketo, na hivyo sentensi nzima. Nafasi ya neno NENI- mara nyingi halina tatizo, hata hivyo litaendelea kukanusha sentensi nzima:

 • La tempo pasinta jam neniam revenos; la tempon venontan neniu ankoraŭ konas. - Muda uliopita kamwe hautarudi tena; kuhusu muda unao kuja hakuna mtu anaejua.

  Muda uliopita hautarudi tena. Hakuna mtu anaejua kuhusu muda ujao.

 • Mi neniel povas kompreni, kion vi parolas. - Hakuna namna ambayo ninaweza kuelewa anacho kisema.

  Siwezi kuelewa

 • La nokto estis tiel malluma, ke ni nenion povis vidi eĉ antaŭ nia nazo. - usiku ulikuwa wa giza kubwa kiasi kwamba hatukuwezi kuona kitu chochote, hata mbele ya pua.

  Hatukuwezi kuona. Kukanusha huathiri kifungu tu cha ke. Kitenzi cha kishazi huru, estis hubakia katika hali kinishi.

 • Neniu radio al mi lumas, neniu varma aereto blovas sur min, neniu amiko min vizitas. - Hakuna mishale inayo angaza kwangu, hakuna upepo wa joto unaovuma, hakuna rafiki anaenitembelea.

  Hakuna mishale inayo angaza.Hakuna upepo unaovuma.Hakuna rafiki anaenitembelea.

 • Memoru, ke Esperanto estas nenies propraĵo. - Kumbuka kwamba Kiesperanto siyo mali ya mtu.

  Kiesperanto siyo mali ya mtu.

 • Tian Regularon por nia Ligo mi nenial povus aprobi. - Sheria hizo na Kanuni za Ligi yetu hakuna sababu kuipitisha.

  Kwa sababu yoyote ile siwezi kuipitisha. Nenial hukanusha sentensi nzima.

Kukanusha mara mbili

Wakati tunatumia neno -NENI, tunapoongeza pia nenone, hivyo sentensi inakuwa yakinishi. Aina hii ya ukanushi wa mara ya plil unaweza kutumika kwa maelezo ya maana ya kipekee sana tu.

 • Mi ne amas neniun. - Sichukii ata mmoja.

  Sio kwamba simpendi mtu. Nampenda mtu.

 • Ĝi ne estas nenies propraĵo. - NI mali mtu.

  Si kwamba haina miliki. Ni mali ya mtu.

Sentensi inaweza kuwa yakinishi kama neno-NENI hukanusha kabisa kitenzi,na lingine neno na -NENI hutokea katika sentensi:

 • Mi ankoraŭ neniam gajnis nenion. = Neniam okazis tio, ke mi gajnis nenion. - Sijahi kutoshindia kitu tena. = Haijatokea nikose kushindia kitu.

  Kila muda huwa nashindia kitu fulani.

Lakini maneno kadhaa ya NENI katika sentensi moja hayana maana ya kuigeuza iwe yakinishi. Mara nyingi hayo maneno huimarishana na ukanushaji unabaki:

 • Ni malutilon alportus al nia afero grandan, kaj utilon ni alportus al neniu nenian. - Tutaleta ufanisi kwa biashara yetu kubwa, hatutaleta manufaa yoyote tutayaleta kwa mtu.

  Hatutaleta ufanisi.

 • Neniam, neniam, neniam li revenos. - Kamwe, kamwe, kamwe hatarudi.

  Yeye hatarudi .Haijalishi moja, mbili, tatu au zaidi ya neniam.

Ukanushi wasehemu

Mara kwa mara, neno ne huonekana kwenye sentensi ili liweze kukana tu sehemu yake. Prediketo inabaki sahihi. Ne inakataa hasa kitu ambacho husimama baada yake, na hilo linaweza kuwa neno linalolifuata moja kwa moja , sentensi inayofuata au hata nyingine. Mazingira ndo inaweza kuonyesha kile ambacho kinakanushwa:

 • Ni faris la kontrakton ne skribe, sed parole. - Tulifanya mkataba siyo wa maandishi, lakini wa maongezi.

  Tulifanya mkataba, lakini siyo wa maandishi.

 • Ne ĉiu kreskaĵo estas manĝebla. - Sio kila mmea inaliwa.

  Ni mimea michache inaliwa. Linganisha na:Ĉiu kreskaĵo ne estas manĝebla.=Neniu kreskaĵo estas manĝebla.

 • Li estas homo ne kredinda. - Yeye ni mtu asiyeaminika.

  Ni mtu

 • En la animo ĉiuj privataj homoj kaj ĉiuj registaroj ne povas ne aprobi nian ideon. - Katika nafsi zao watu wote binafsi na serikali zote haziwezi kupinga idhini yetu.

  ne ya kwanza inathiri prediketo povas na hukanusha sentensi nzima. ne yaathiri aprobi tu. Maana ya jumla ni: Ili ne povas rifuzi nian ideon. (Hawawezi kukataa maoni yetu.) = Ili devas aprobi nian ideon. (Wanapaswa kuidhinisha mawazo yetu. )

Maneno ya NENI kwa ujumla hayanakanusha sentensi yote bila kujali oda ya maneno, lakini wakati mwingine neno la NENI linaweza kuwa halali kwa sehemu tu ya sentensi. Kisha mazingira na oda lazima yaweke wazi hilo:

 • Mi decidis paroli jam plu nenion pli pri tiu ĉi temo. - Niliamua kutosema tena kitu kuhusu mada hii.

  Uamuzi ni wa kweli. Kukataa huathiri tu kusema na maneno yote yanayohusiana nayo moja kwa moja.

 • Pli valoras faro nenia, ol faro malbona. = Faro, kiu ne okazis, ja valoras pli, almenaŭ kompare kun faro malbona. - Kitendo chenye chenye hakipo kina thamani kuliko kitendo kibaya. = Hatua ambayo haikutokea inafaa zaidi angalau ikilinganishwa na hatua mbaya.

  Prediketo valoras inabaki yakinishi.

Wakati ne au neno na NENI ni sehemu ya neno la mchanganyiko, basi ukanushaji una maana tu ndani ya neno hilo:

 • Sinjoro, vi estas neĝentila. - Bwana, wewe hauna adabu.

  Sentensi hiyo husema kuwa bwana huyo bila shaka ana tabia, ambayo ni ukosefu wa adabu. Hii ni tofauti kidogo na: Hauko muungwana.

 • La pastro, kiu mortis antaŭ nelonge (aŭ antaŭ nelonga tempo), loĝis longe en nia urbo. - Mchungaji aliyekufa hivi karibuni (au muda mfupi uliopita), aliishi kwa muda mrefu katika mji wetu.

  Ukanushi unahusiana tu urefu wa muda.

 • Bedaŭrinde ili estas ne-Esperantistoj. - Kwabahati mbaya si Waesperantiste.

  Ni watu ambao hawajui Kiesperanto.

 • Neniofarado estas tre dolĉa okupo. - Kukosa chakufanya ni vizuri.

  Muda ule ambao hufanyi chochote,ni mtamu sana.

Nek

Nek inamaanisha "na pia si" (wala). Inatumiwa baada ya kutumia ne, unapotaka kukanusha tena kitu. Ni kama kibadilishaji cha kaj, na kimsingi hufuata sheria sawa na kaj:

 • Li ne vidis min, nek aŭdis. = ...kaj ankaŭ ne aŭdis. - Hakuniona mimi, wala hakunisikia. = ... na pia hakuweza kunisikia.
 • Mi ne renkontis lin, nek lian fraton. = ...kaj ankaŭ ne lian fraton. - Sikukutana na yeye wala kaka yake.=...na wala kaka yake.
 • Nenia peno nek provo donos lakton de bovo. - Jitihada wala jaribio halitatoa maziwa kutoka kwa ng'ombe.

Usitumie nek kuunganisha vitu viwili baada ya sen. Tumia kaj: Tiu virino ne foriru de ŝi sen konsolo kaj helpo. Ne: ...sen konsolo nek helpo.

Nek si sawa na ne + msisitizo. Ili kusisitiza kabisa kukanusha, tumia pamoja na ne. Usiseme: Mi havas nek unu amikon. Sema: Mi havas eĉ ne unu amikon. Au: Mi ne havas unu amikon.

Unaweza pia kusema, nek iliozidishwa au changwa changwa.

Kurudi juu