Kwa maudhui

Maswali na KI

Maswali na KI yanajengwa kwa correlative na KI . Maswali ya KI huwakilisha habari ambazo mtu anatafuta.

Neo na KI kawaida husimama mwanzo wa kifungu cha swali:

  • Kion vi volas?Mi volas manĝon! - Unahitaji nini?-Nahitaji chakula!
  • Kian manĝon vi deziras?Mi deziras malmultekostan manĝon! - Ni chakula cha aina gani ungependelea?-Ningependelea chakula cha bei chini!
  • Kiel vi fartas?Mi fartas bone! - Habari yako? - Mimi ni mzima!
  • Kiom da pomoj vi havas?Mi havas du kilogramojn da pomoj! - Una tofaa ngapi? - Nina kilo mbili za tofaa!
  • Kies estas tiu aŭto?Ĝi apartenas al Anno! Ĝi estas de Anno! Ĝi estas ŝia! - Mwenye gari hii ni yupi? -Ni ya Anna!Ni ya Anna! Ni yake!
  • Kiam do?Morgaŭ! - Wakati gani tena? -Kesho!

Maneno na KI yanatumika pia katikavishazi tegemezi vya maswali:Ŝi demandis, kion mi volas.

Maswali na Ĉu

Maswali na Ĉu yanajengwa kwa neno la kuuliza Ĉu. Swali na Ĉu linaomba uthibitisho wa usahihi wa sentensi nzima. Jibu kawaida ni jes (ndiyo) au ne .(hapana).

Ĉu kawaida huja mwanzoni mwa sentensi na swali:

  • Ĉu vi komprenas min?Jes, mi komprenas vin! Ne, mi ne komprenas vin! - Je! Umenielewa? -Ndiyo, nimekuekewa! Hapana,Sijakuelewa!
  • Ĉu vi estas Kanadano?Jes, mi estas Kanadano! Ne, mi ne estas Kanadano! - J! Wewe ni Mkanada? - Ndiyo, mimi ni Mkanada! Hapana, mimi siyo Mkanada!
  • Ĉu li?Jes, li! - Je! yeye? - Ndio, yeye!
  • Ĉu ĝi estas taŭga?Jes, (ĝi) estas! - Je! Inafaa? - Ndiyo inafaa!

Swali na Ĉu pia linaweza kutumika kwa sentensi na maswali mengi ya kuchagua. Katika hali hiyo, jibu kawaida unachaguzi kati ya njia mbalimbali zilizowasilishwa:

  • Ĉu vi volas kafon aŭ teon?Mi volas kafon! Mi volas teon! Mi volas nek kafon, nek teon! Mi volas kaj kafon, kaj teon! - Unahitaji kahawa au chai? -Nahitaji kahawa!Nahitaji chai! Sihitaji kahawa wala chai! Nahitaji vyote kahawa na chai!
  • Ĉu li aŭ ŝi?Ŝi! Li! Iu ajn el ili! Neniu el ili! Ambaŭ! - Je! Yeye (mwanaume) au yeye (mwanamke)? - Yeye, mwanamke! Yeye, mwanaume! Aidha mmoja wao! Hakuna hata mmoja wao! Wote!

Maneno ya majibu

Kujibu maswali na ĉu, unaweza kusema sentensi (kamili au iliyofupishwa) inayoweza kutoa jibu kwa swali:

  • Ĉu vi amas min? — Mi amas vin! - Unanipenda? — nakupenda!
  • Kaj ĉu vi longe lernis? — Ho, mi lernis ne malpli ol tri jarojn. - Na umeweza kusoma kwa muda mrefu?— Oh, nilisoma siyo chini ya miaka mitatu.

Lakini kwa kawaida tunatumia maneno jes (ndiyo) na ne (hapana) kama majibu. Maneno hayo ni kama sentensi nzima peke yake, hufanya kama sentensi kamili. Mara nyingi baada ya maneno ya jibu unaongeza sentensi nzima ya jubu au sehemu ya sentensi ya aina hiyo kwa ufafanuzi wa ziada.

Jes

Neno la kujibujes (ndiyo) hutoa jibu chanya:

  • — Ĉu vi volas kafon? — Jes! (= Mi volas kafon.) - — Unahitaji kahawa? — Ndiyo!(=Nahitaji kahawa.)
  • — Ĉu vi ion deziras? — Jes! (= Mi ion deziras.) - — Ungependelea kitu chochote? — Ndiyo (=Ningependelea kitu.)
  • Ĉu la Universala Kongreso estos en Eŭropo ĉi-jare? — Mi pensas, ke jes! = Mi pensas, ke ĝi ja estos en Eŭropo ĉi-jare! - Je! Kongamano lakimataifa litafanyika Ulaya mwaka huu? — Nadhani hivyo! = Nadhani itakuwa Ulaya mwaka huu!

    Neno la kujibu jes linachukua nafasi ya kishazi tegemezi (ukiacha ke ya utangulizi.

Usitumie jes katikati ya sentensi kwa kusisitiza ukweli wa kitu fulani. Kwa hiyo tumia neno ja. Usiseme: Tiu ĉi suko ne estas dolĉa, dum tiu alia jes estas. Sema: Tiu ĉi suko ne estas dolĉa, dum tiu alia ja estas. (Juisi hii si tamu, pindi hiyi nyingine ni tamu.

Ne

Neno ne{2] hutoa jibu la kukanusha:

  • — Ĉu vi volas kafon? — Ne! (= Mi ne volas kafon.) - — Unahita kahawa? — Hapana! (=Hapana sihitaji kahawa.)
  • — Ĉu vi ion deziras? — Ne! (= Mi nenion deziras.) - Unapndelea chochote?-Hapana! Sihitaji kitu chochote.)
  • Ĉu li estas blondulo aŭ brunulo? — Ne, pli kaŝtanhara. = Li estas nek blondulo nek brunulo, li estas pli kaŝtanhara. - Je, yeye ana nywele zamanjano au nywele za rangi yakunde? — Hapana, ni chestinati zaidi. = Hana nywele nyekundu za rangi ya kunde, nywele zake ni rangi zaidi ya chestinati.
  • Ha, ĉu efektive la malgranda Kay mortis? La rozoj estis sub la tero, kaj ili diras, ke ne! = ...ili diras, ke li ne mortis. - Oh, hakika dogo Kay alifariki? Waridi zilikuwa chini ya ardhi na wakasema hapana! = ... walisema kwamba hakufa.

Ni muhimu kuzingatia tofauti kati ya ne (si) kama neno la kukanushaa ndani ya sentensi, na ne (hapana) kama jibu la swali :

  • Ne venu ĉi tien! = Mi volas, ke vi ne venu ĉi tien. - Usije hapa! =Sihitaji wewe uje hapa.

    Ne inakataa prediketo.

  • Ne, venu ĉi tien! = Ne! Mi ja volas, ke vi venu ĉi tien. - Hapana, njoo hapa!= Hapana! Nataka uje hapa.

    Ne ni neno la kujibu na lina jukumu kidogo kama sentensi nzima.

Ikiwa moja kwa moja baada ya ne ya kujibu inafuata sentensi inayoanza na kitenzi, unapaswa kutamka na kuweka pumziko la wazi baada ya ne ili uepuke kutokuelewana.

Jes na nekatika maswali ya kukanusha

Kuna njia mbili za kutumia maneno ya majibu kwa maswali yakukanusha. Mfumo mmoja ni wa kawaida zaidi katika lugha za Magharibi, na mwingine ni wa kawaida zaidi katika lugha za Mashariki. Kwa hiyo, mtu anaweza kusema juu ya matumizi yaMagharibi na Mashariki, lakini kwa kweli, katika nchi nyingi na lugha nyingi, mifumo yote hutumiwa kwa pamoja. Mfumo huo upo kwa Kiesperanto pia. Zamenhof alitumia maranyingi jes (ndiyo) na ne (hapana) hasa kulingana na mfumo wa Magharibi, lakini pia alitumia mfumo wa Mashariki mara nyingi.

Mfumo wa Magharibi

katika mfumo wa magharibi, jes huwakilishwa nasentensi za majibu ya chanya, na ne huwakilisha sentensi za majibu ya kukanusha. Sentensi za majibu ya kukanusha ni yenye sentensi na neno la ukanushi (ne (si) au neno na NENI) katika sehemu ya kishazi huru. Katika mfumo wa Magharibi, maana ya neno la kujibu halitegemei mfumo wa swali. Ikiwa swali ni hasi, majibu yanatolewa kwa neno hilo hilo la kujibu ambalo litatumika ikiwa swali halikuwa na neno la kukataa. Jambo muhimu tu ni fomu ya hiyo sentensi ya jibu ambayo inawakilishwa na neno la kujibu:

  • Ĉu vi volas kafon? - Unahitaji kahawa?(swali chanya)
    • Jes! (= Mi volas kafon.) - — Ndiyo!(=nahitaji kahawa.)
    • Ne! (= Mi ne volas kafon.) - — Hapana!(=Sihitaji kahawa.)
  • Ĉu vi ne volas kafon? - Hauhitaji kahawa?(swali la kukanusha)
    • Jes! (= Mi volas kafon.) - — Ndiyo!(=nahitaji kahawa.)
    • Ne! (= Mi ne volas kafon.) - — Hapana!(=Sihitaji kahawa.)
  • Ĉu vi nenion deziras? - Kuna kitu chochote kile ambacho unahitaji?
    • Jes! (= Mi ja deziras ion.) - — Yes! (=naweza kuhitaji kitu.)
    • Ne! (= Mi deziras nenion.) - — Hapana! (=Nahitaji kitu.)

Ili kujibu swali la kukanusha (katika mfumo wa Magharibi) kwa jibu la kukubali, unaweza pia kutumia jibu la kusisitiza Jes kabisa! = Jes, ndiyo hakika (au kitu kama hicho):Ĉu vi ne volas trinki la malvarman kafon? (Je! wewe hautaki kunywa kahawa ya baridi?) — Jes ja! (Ndio kabisa) (= Jes, mi ja volas trinki ĝin.) (Ndio nahitaji kuinywa kabisa) Wangine wanatumia tamen anstataŭ jes ja.

Mfumo wa magharibi

Katika mfumo wa mashariki jes inathibitisha hasa yaliyomo ya swali, na ne inakat sentensi yote ya kuhoji. Katika mfumo huu, jes na ne hubadilishana jukumu katika maswali ya kukanusha:

  • Ĉu vi volas kafon? - Unahitaji kahawa?(swali chanya)
    • Jes! (= Mi volas kafon.) - — Ndiyo!(=nahitaji kahawa.)
    • Ne! (= Mi ne volas kafon.) - — Hapana!(=Sihitaji kahawa.)
  • Ĉu vi ne volas kafon? - Hauhitaji kahawa?(swali la kukanusha)
    • Jes! (= Mi ne volas kafon.) - — Ndiyo! (=Sihitaji kahawa.)
    • Ne! (= Mi ja volas kafon.) - — Hapana! (=Nahitaji kahawa.)
  • Ĉu vi nenion deziras? - Kuna kitu chochote kile ambacho unahitaji?
    • Jes, mi nenion deziras. - — Ndiyo, sihitaji chochote.
    • Ne, mi ja deziras ion. - -Hapana, nahitaji kitu.

Mifumo miwili ya mantiki.

Mifumo yote miwili ya kujibu maswali ya kukanusha, ni maantiki lakini kwa njia tofauti. Ingekuwa vizuri kama pangekuwa mfumo mmoja tu katika Kiesperanto. Kwa kweli, mfumo wa Magharibi unaweza kupendekezwa, kwa sababu hadi sasa hutumiwa mara nyingi, na pia ni wazi zaidi kwa Zamenhof. Lakini inaonekana kwamba inaweza kuwa haiwezekani kufikia matumizi ya mfumo mmoja kabisa. Matumizi yote mawili ni yanakubalika. Ni lazima kuwa makini katika kujibu maswali yaliyo katika kauli yakukanusha. Ni muhimu kuongeza sentensi ya kujibu ya wazi zaidi ili kuepuka na hatari ya kutokuelewana.

Kurudi juu