Neno po linaonyesha usambazaji wa idadi. Mwanzo ilikuwa inachukuliwa kama kihusishi, lakini wengi huitumia kama kielezi.
Po ina maana tu kuhusiana na idadi yoyote au kiasi. Baada ya po daima panafuata neno la idadi au neno lingine la wingi: po kvin, (tano tano) po dek (kumi kumi), po dudek mil (ishirini ishirini elfu), po multe, (wengi wengi) po kiom, (wangapi wangapi) po miliono (milioni milioni), po duono, (kipande kipande/nusu nusu)po iom (kiasi kiasi), po pluraj (wengi wengi), po paro (jozi jozi), po egalaj partoj(sehemu zakulingana lingana) k.s. mara nyingine usakiye kwa mbali idadi: po pomo = po unu pomo (tofaa moja moja), po tutaj boteloj = po pluraj tutaj boteloj (machupa yote yote).
Po inaonyesha sehemu ya kitu fulani ambacho kimesambazwa kwa watu kadhaa, kwa mambo kadhaa, kwa maeneo kadhaa au mazingira kama hayo. Kila moja ya vitu tofauti ni sehemu moja. Ili kupata idadi yote kwa jumla, ni muhimu kuzidisha po idadi ya makundi. Idadi hiyo inategemea mazingira:
-
Por miaj kvar infanoj mi aĉetis dek du pomojn, kaj al ĉiu el la infanoj mi donis po tri pomoj. - Kwa watoto wangu wanne nilinunua tofaa kumi na mbili, na kila mmoja nilimpa tofaa tatu tatu.
Tofaa 3 kuzidisha 4 = tofaa 12 . Kumbuka kuwa matokeo huonyesha tofaa, si watoto. Tulizidisha tofaa 3 kwa idadi ya watoto, lakini matokeo yake ni tofaa 12 , si watoto 12. Matokeo ya hesabu hii daima yanahusiana na yale ambayo po inaonyesha.
-
Tie estis viro tre altkreska, kiu havis sur la manoj kaj sur la piedoj po ses fingroj, sume dudek kvar. - Kulikuwa na mtu mrefu sana, ambaye alikuwa na vidole sita sita kwenye kiganja na miguu, jumla ya ishirini na nne.
Vidole 6 kuzidisha 4 (mikono 2 + miguu 2) = vidole 24.
-
Tiu ĉi libro havas sesdek paĝojn; tial, se mi legos en ĉiu tago po dek kvin paĝoj, mi finos la tutan libron en kvar tagoj. - Kitabu hiki kina kurasa sitini; Kwa hiyo, ikiwa nitasoma kila siku kurasa kumi kumi na tano, nitamakiza kitabu hicho kwa siku nne.
Kurasa 15 kuzidisha 4 = kurasa 60.
-
Ŝi ricevis lecionojn po dek eŭroj por horo. - Alipata somo kwa euro kumi kumi kwa saa.
Ikiwa masomo yalimaliza kwa ujumla, kwa mfano masaa 4, gharama ilikuwa: euro 10 kuzidisha 4 = euro 40.
-
Dume la gastoj trinkis po glaseto da vino. - Wakati huo huo, wageni walinywa glasi moja moja ya divai.
Hapa neno moja halisikiki: ... moja moja glasi ... Kama kulikuwapo kwa mfano Wageni 10, ujumla kulikuwa na glasi 10.
-
Mi fumadis cigaredojn po dudek kvin rubloj por cento. - Nilivuta sigara za lebasi ishirini ishirini na tano kwa mia (kwa sigara mia) .
sigara mia ina thamani ya lebasi 25 . Kwa mfano mia 5 ya sigara hizi ina gharama ya: lebasi 25 kuzidisha 5 = lebasi125.
-
El ĉiuj vivaĵoj, el ĉiu karno, enkonduku po unu paro el ĉiuj en la arkeon, ke ili restu vivaj kun vi. - Kutoka kwa viumbe vyote, kutoka kwa mwili wote, ingiza jozi moja moja ndani ya safina ili vibaki hai na wewe.
Ikiwa ilikuwa Aina 1000 za wanyama, kutakuwa na wanyama 2 (jozi 1) kuzidisha1000= 2000 (jozi 1000).
-
La urbestro aranĝas grandajn tagmanĝojn, kie la vino estas trinkata po tutaj boteloj. = ...po pluraj tutaj boteloj. - Meya hupanga chakula cha mchana, ambapo divai inatumiwa kwenye machupa yote = ... machupa yote.
Katika chakula hiki cha mchana wanakunywa machupa mengi yote.
Katika mifano iliyotangulia po hutumiwa kama kihusishi. Katika maelezo ya idadi kuna mifano ya po inayotumika kama kielezi.
Matumizi mabaya ya po
Mara nyingi po inawekwa kabla ya msemo mbaya. Ona mfano:
-
Tiu ĉi ŝtofo kostas dek dolarojn po metro.
Msemaji alitaka kusema kwamba kila mita ya kitambaa huuzikana dola kumi, lakini hiyo si sahihi. Po hapa lazima ihusiane na moja kwa mita moja isiosikika vizuri. Mahesabu inafanywa: mita 1 kuzidisha ya 10 (idadi ya dola) = 10 mita . Katika sentensi hii po inaonekana kabla ya maneno (moja) mita. Matokeo ya hesabu hiyo ni mita kumi, sio dola kumi. Hizi mita kumi za kitambaa zina thamani ya ya dola kumi jumla. Hii inamaanisha kwamba kila mita inauzikana dola moja. Hili bila shaka sio maana iliyotarajiwa.
Sentensi sahihi ni:
-
Tiu ĉi ŝtofo kostas po dek dolarojn por metro. - Kitambaa hiki kinauzikana dola kumi kwa mita moja.
Ikiwa kuna Mita 5, hesabu inafanywa: dola 10 kuzidisha 5 = dola 50. Sasa matokeo inaonyesha dola kwa sababu po inasimama kabla ya maneno dola kumi.
Lugha nyingi hutumia neno moja tu la kuonyesha mgawanyiko. Neno hili linasimama kabla ya mita. unasimamisha po na maneno kama hayo yenye maana nyingine kabisa kuliko po. Kwa Kiesperanto, mambo haya yanaelezwa kwa maneno mawili, po na nyingine. Neno lingine mara nyingi ni por, lakini kulingana na mazingira pia vihusishi mengine (au mfumo wa vihusishi) yanaweza kutumika. Katika mfano ulioandikwa hapo juu inaweza kuwa laŭ metro au mitre .
Angalia pia tofauti kati ya sentensi zifuatazo:
-
La aŭto veturis po dek kilometrojn en kvin horoj. - Gari hiyo ilikuwa mbio kilomita kumi kumi katika masaa tano.
Gari alisafiri kwa jumla ya masaa 5, na safari kwa jumla ya kilomita 50. (Kilomita 10 kuzidisha 5 = kilomita 50.)
-
La aŭto veturis dek kilometrojn en po kvin horoj. - Gari lilikimbia kilomita kumi katika masaa tano tano.
Gari lilienda kwa jumla ya kilomita 10, ambayo ilidumu kwa jumla ya masaa 50. (Masaa 5 kuzidisha 10 = 50 masaa.)
Fomula zenye kistarungio
Fomula | Neno |
---|---|
20$/kg | po dudek dolaroj por kilogramo |
120 km/h | po cent dudek kilometroj en/por horo |
2 MN/m² | po du meganeŭtonoj sur/por kvadratmetro |
Mara nyingi mtu anaweza pia kutumia po pamoja na kielezi: po 120 kilometroj hore.
Mara kwa mara mtu anaweza kuondoa po kwa maneno kama hayo, kwa kuongeza ĉiu (kila), kwa mfano: kilomita mia ishirini kwa kila saa (kila) saa , dola ishirini kwa kila kilo , meganeutoni mbili kwa (kila) mita ya mraba.