Kwa maudhui

Vihusishi ni maneno yaliyowekwa kabla ya misemo ili kuonyesha umuhimu yao katika sentesi.

Vihusishi kawaida huja kabla ya nomino au viwakilishi , lakini pia kabla ya vitenzi kwenye infinitive , na sentensi changamano au ambatano[8}. Wakati mwingine vihusishi hutumiwa kabla ya vielezi vya mahali na vya muda. Vihusishi kipindi hico huonyesha maana ya mahali na muda.

Maneno yfuatayo ni vihusishi: al, anstataŭ, antaŭ, apud, ĉe, ĉirkaŭ, da, de, dum, ekster, el, en, ĝis, inter, je, kontraŭ, krom, kun, laŭ, malgraŭ, per, po, por, post, preter, pri, pro, sen, sub, super, sur, tra natrans:

Vihusishi tegemezi

Baada ya kihusishi kawaida kuna maneno ambayo kihusishi inahusiana. Bila maneno yafuatayo, kihusishi hakina maana: sur la tablo, en mia domo, ekster tiu ĉi ĉambro, dum la paŭzo, anstataŭ tio, krom Petro n.k.

Ikiwa unataka kuacha maneno baada ya kihusishi (kuyapuuziya), unatakiwa utumie kihusishi na mwisho E, kwa sababu kipindi hicho kihusishi kinakuwa ni sehemu ya sentensi ambayo ina umuhimu kama kielezi:

  • Li staras apud mi.Li staras apude. - Yeye yupo karibu nami. → Yeye yupo karibu.
  • Ŝi sidas ekster la domo.Ŝi sidas ekstere. - Yeye ameketi nje ya nyumba. → Yeye ameketi nje.
  • Tio okazis dum la paŭzo.Tio okazis dume. - Hilo lilitokea wakati wa mapumziko. → Hilo lilitokea wakati huu.
  • Tio okazos post la kongreso.Tio okazos poste. - Hilo litakuwa baada ya kongamano. → Hilo litakuwa baadae.

Kama kielezi kinaonyesha mahali, inaweza kuchukua N mwisho kwa kuonyesha harakati ya kuelekea mahali:

  • Li sidas ekster la domo.Li sidas ekstere.Li iras eksteren. = ...al ekstera loko (al loko ekster la domo). - Yeye ameketi nje ya nyumba. → Yeye ameketi nje. → Anatoka nje. = ... katika tovuti ya nje (mahali nje ya nyumba).

Ikiwa kwa wakati mwingine kifungu cha awali kinafanya kazi kama kivumbuzi, mwisho wa A unatumiwa baada ya maonyesho:

  • Li loĝas en domo apud mia domo.Li loĝas en apuda domo. ...en domo apuda. - Anaishi katika nyumba karibu na nyumba yangu. → Anaishi katika nyumba iliyo karibu. ... katika nyumba jirani.

Lakini unaweza pia kutumia kielezi cha nafasi au cha muda katika kesi kama hizo: Li loĝas en domo apude. = Li loĝas en domo, kiu troviĝas apude.

Kwa sababu fulani baadhi ya vihusishi ambavyo vina mwisho wa E au mwisho A. Kwa mfano hauwezi kusema paroli prie = "kuzungumzia hicho", iri dee = "kuondoka umetoka sehemu", ala veturo = "kuelekeya panapolengwa ", proa agado =" kazi kwa ajili ya hicho".

Kurudi juu