Kwa maudhui

Kiwakilishi ni neno ambalo linaweza kuchukua nafasi ya nomino ndani ya sentensi.

viwakilishi nafsi.

mi
= "msemaji"
ni
= "msemaji na wengine watu"
vi
≈ wasikilizaji
li
≈ "mtu wa kiume au mtu mwenye jinsia isiyojulikana"
ŝi
≈ "mtu wakike anayesemwa"
ĝi
≈ kitu kinachosemwa, mnyama au katoto"
ili
≈ "watu wanaosemwa, vitu, au wanyama"
oni
≈ "watu wasiowekwa wazi"
si
≈ "mtu huyo huyo kama kiima", ikiwa si mi , ni au vi

Viwakilishi nafsi vinaweza kupokea mwisho N wa accusative:

 • Mi amas vin. - Ninakupenda wewe.
 • Ilin konas Karlo. - Charles anawajua .
 • Ĉu vi ĝin vidas? - Je,wewe uliiona?
 • Elizabeto lavas sin en la lago. - Elizabeth anajisafisha mwenyewe kwenye ziwa.

Viwakilishi vimilikishi

Ikiwa tunaongeza mwisho A kwa viwakilishi nafsi, tunafanya viwakilishi milikishi :

mia
"...cha mimi"
nia
"(cha)...cha sisi"
via
" ... ya wewe"
lia
"... ya yeye"
ŝia
" ... ya"
ĝia
" ... ya"
ilia
" ... yao"
onia
"... yako/ yetu"
sia
" ...yake mwenyewe"

Viwakilishi milikishi vinaweza kupokea mwisho J na N kama vivumishi vingine : mia ĉambromiaj ĉambrojmian ĉambronmiajn ĉambrojn.

Kama kiwakilishi milikishi kinaonekana kabla ya nomino, ni difinilo, na hauongezi la . kiwakilishi milikishi kinaelezea mmiliki, na hiyo ni habari ya kutosha ili kuonyesha usahihi. Ikiwa unaweka demsemo badala ya kiwakilishi milikishi mtu lazima aongeze la: ilia ĉambro = la ĉambro de ili, mia edzo = la edzo de mi.

Wakati kiwakilishi milikishi knaonekana peke yake bila jina baadae, sio kitambulishi, na hakionyeshi maana utambulisho. Ili kuonyesha utambulisho unaongeza la:

 • Tiu ĉi libro estas mia. - Kitabu hiki ni changu. .

 • Tiu ĉi libro estas la mia. - Kitabu hiki ni changu.

 • Mia aŭto estas difektita. Ni provu la vian. La vian = vian aŭton. - Gari yangu imeharibiwa. Tujaribu yako. Yako = gari lako.

Lakini wakati mwingine, hii la inaweza kuachwa kabla ya kiwakilishi milikishi, ikiwa maana iko wazi sana:

 • Li pli ŝatas mian domon ol (la) sian. = ...ol sian domon. - Anapenda nyumba yangu zaidi kuliko yake. = ... kuliko nyumba yake.

Viwakilishi vingine

Pia maneno mengine ni viwakilishi (lakini sio nafsi), kwa mfano. orodha ya maneno yenye O, U na ES na neno ambaŭ.

Mtu wa kwanza

Mi

Mi ni ya umoja(na haionyeshe jinsia). Mi na mia hutumiwa na msemaji kujieleza wenyewe. Kwa sarufi hii mara nyingi huitwa "mtu wa kwanza":

 • Mi venas de la avo, kaj mi iras nun al la onklo. - Nimekuja kutoka kwa babu, na sasa ninaenda kwa mjomba.
 • Mi foriras, sed atendu min, ĉar mi baldaŭ revenos. - Mimi ninaondoka, lakini unisubiri, kwa maana nitarudi hivi karibuni.
 • Por miaj kvar infanoj mi aĉetis dek du pomojn. - Nilinunulia tofaa (apples) kumi na mbili kwa watoto wangu wanne.
 • Kiam mi finos mian laboron, mi serĉos mian horloĝon. - Ninapomaliza kazi yangu, nitatafuta saa yangu.
 • Mi prenos miajn glitilojn kaj iros gliti. - Nitawachukua kipungu changu na nitaenda kutereza.

Ni

Ni ni wingi (na haionyeshi jinsia hata kidogo). Ni na nia hutumiwa na msemaji kujieleza yeye mwenyewe na mtu mwingine. Ni inaweza kumaanisha mimi na mtu mwingine mmoja , mimi na watu wengine kadhaa , mimi na watu wengine wote , au mi na wewe . Kiwakilishi ni hapa kinajumuisha watu wanaoelezewa, sio. Wale waliojumuishwa wanaweza kuonyesha tu maana:

 • Ni vidas per la okuloj kaj aŭdas per la oreloj. - Tunaona kwa macho na kusikia kwa masikio.

 • Ni disiĝis kaj iris en diversajn flankojn: mi iris dekstren, kaj li iris maldekstren. - Tulisambaa na kwenda njia tofauti: Nilikwenda kulia, na akaenda kushoto.

  Ni = "mimi na yeye".

 • Kiam vi ekparolis, ni atendis aŭdi ion novan, sed baldaŭ ni vidis, ke ni trompiĝis. - Ulipozungumza, tulisubiri kusikia kitu kipya, lakini upesi tuliona kwamba tulidanganywa.

  Ni = "Mimi na wengine, lakini siyo wasikilizaji".

 • La nokto estis tiel malluma, ke ni nenion povis vidi eĉ antaŭ nia nazo. - Usiku ulikuwa wa giza sana kwamba hatukuweza kuona chochote ata mbele ya pua zetu.
 • La junulo aliĝis al nia militistaro kaj kuraĝe batalis kune kun ni kontraŭ niaj malamikoj. - Mvulana huyo alijiunga na jeshi letu na kwa ujasiri alipigana nasi dhidi ya adui wetu.
 • Kiam vi vidis nin en la salono, li jam antaŭe diris al mi la veron. - Wakati ulipotuona saluni, alikuwa ameniambia ukweli.

  Ni = "mimi na yeye".

Nafsi yapili

Vi

Vi na via hutumiwa na msemaji kuzungumza juu ya mtu ambaye anasema. Vi na via pia inaweza kuhusu watu wengine ambao kwa namna fulani ni wanakundi moja kama wasikilizaji. Kwa sarufi hii inaitwa "nafsi ya pili". vi hutumiwa sawa kwa mtu mmoja au zaidi. Vi ni nafsi yapili umoja na wingi. Vi haionyeshi jinsia hata kidogo, na pia ni neutral kabisa kuhusu cheo au nafasi k.t.p:

 • Sinjoro, vi estas neĝentila. - Muheshimiwa, wewe si mwungwana.
 • Sinjoroj, vi estas neĝentilaj. - Bwana, wewe si mwungwana.
 • Vi estas infanoj. - mko watoto.
 • Ĉu vi amas vian patron? - Unampenda baba yako?
 • Via parolo estas tute nekomprenebla kaj viaj leteroj estas ĉiam skribitaj tute nelegeble. - Kuzungumza kwako hakueleweki kabisa na herufi zako kila mara hazisomeki.
 • Sidigu vin, sinjoro! - kaa, bwana!

Wakati vi ni kiima cha kitenzi ambacho kina mwisho U, kwa kawaida huachwa .

Katika lugha zingine, kiwakilishi kama vi hutumiwa kuzungumza juu ya watu kwa ujumla. Kwa hiyo katika Kiesperanto, unatumia kiwakilishioni.

Ci

Ci (wewe) ni kiwakilshi cha umoja kwa kuonyesha mtu, ambayo haionyeshi jinsia. Ci (wewe) na cia (zako) ziko katika kanuni tu, na hazijawahi kutumiwa. Inawezekana kufikiri ci kama ya umoja tu vi, au kama kiwakilishi cha kifamilia (umoja) vi, au kama tusi (umoja) vi. Lakini kwa kweli, haiwezekani kusema inaonyesha uhusiano gani, kwa sababu haitumiwi. Watu wengine wanafikiri kwamba ci ilitumika hapo awali kwa Kiesperanto, na kwamba matumizi haya baadaye yamepotea, lakini kwa kweli, ci haijawahi kutumika. huonekana tu mara kwa mara katika matumizi ya majaribio ya lugha, na kadhalika. Katika Kiesperanto a kawaida, nenovi pekee limekuwa likitumiwa mara kwa mara kama kiwakilishi kwenye mazungumzo.

Nafsi ya tatu

Kile kambacho si mi, ni au vi (au ci ), "nafsi ya tatu". Viwakilishi li , ŝi , i na ili , na lia , ŝia , ĝia , ilia , hutumiwa kuzungumza juu ya kitu kinachojulikana, ambacho si msemaji wala msikilizaji. Oni na onia hutumiwa kuzungumza juu ya watu wasiowekwa wazi. Si na sia zinachukuwa nafasi za viwakilishi vya nafsi (nafsi ya tatu) kwa mazingira yalio halisi.

Likajŝi

Li ​​ na ŝi ni ya umoja. Li ​​ na lia hutumika wakati wa kuzungumza juu ya mtu mmoja wa kiume. Ŝi na ŝia hutumiwa wakati wa kuzungumza juu ya mtu mmoja wa kike.

 • Li estas knabo, kaj ŝi estas knabino. - Yeye ni mvulana na yeye ni msichana.
 • Li estas mia onklo. - Yeye ni mjomba wangu.
 • Ŝi estas mia onklino. - Yeye ni shangazi yangu.
 • En la salono estis neniu krom li kaj lia fianĉino. - Sebuleni hapakuwa na mtu isipokuwa yeye na mchumba wake.
 • Mi renkontis vian patrinon kaj ŝian kolegon. - Nimekutana na mama yako na mwenzake.

Wakati tukizungumza juu ya mtu ambaye jinsia yake haijulikani, au wakati tukizungumza kwa ujumla juu ya mtu wa jinsia yoyote ile, tunatumia li. Li Ina maana mbili: mtu wa kiume au mwanadamu :

 • Ĉiu, kiu ŝin vidis, povis pensi, ke li vidas la patrinon. - Kila amuonae yeye hudhani kuwa amemuona mama yake.

  Hapaanajibu kila mtu, kwa hiyo kila mtu.

 • Se vi iros al kuracisto, li povos helpi vin. - Kama ukienda kwa mganga,ataweza kukusaidia.

  Hii inaweza kuwa mganga yeyote bila kujali jinsia.

Matumizi haya ya li yanaonekana kwa wengine kama ubaguzi wa kijinsia, lakini ni kweli tu ya sarufi. Tukitumia li si kwa sababu tunawapuuza wanawake, lakini ni kwa sababu li { 2} ina maana mbili: jinsia ya kiume, na jinsia ya neutral. Hii inaweza wakati mwingine kusababisha mashaka. Katika hali hiyo usisite kueleza kwa wazi kwa mfano ŝi aŭ li, tiu, tiu persono n.k.

Kumbuka: Kuna watu walipendekeza viwakilishi vipya ili vichukuwe nafasi ya kati ya matumizi neutral ya li. Kila konsonanti huru ilabu + "i" tayari imependekezwa ila matumizi yake ni machache. Lakini siku hizi unaweza kuona mara kwa mara ŝli kaj ri, pindi wengine wanasisitiza gi au ĵi au nyingine tena.

Ĝi

Ĝi ni kwa umoja. Ĝi na ĝia hutumiwa kuzungumza juu ya kitu bila jinsia:

 • La tranĉilo tranĉas bone, ĉar ĝi estas akra. - Kisu kinakata vizuri kwasababu ni kikali.
 • Trovinte pomon, mi ĝin manĝis. - Baada ya kupata tufaa, nililila.
 • Mi disŝiris la leteron kaj disĵetis ĝiajn pecetojn en ĉiujn angulojn de la ĉambro. - Nimeichanaa barua na nikatawanya vipande vyake katika pembe zote za chumba.

Tunatumia pia ĝi tunapozungumza juu ya mtoto mchanga sana kwamba jinsia yake si muhimu. Lakini unaweza pia kutumia li kama tunavyofanya kwa watu jinsia zao hazijulikani:

 • La infano ploras, ĉar ĝi volas manĝi. - Mtoto analia kwasababu anataka kula.
 • Mi montris al la infano, kie kuŝas ĝia pupo. - Inaonyesha mtoto wake ulipolazwa mdoli wake.

kama unataka hasa kuonyesha jinsia ya mtoto, au wakati wa kuzungumza juu ya mtoto mkubwa, basi kwa kweli utumie li au ŝi .

Ĝi pia hutumiwa wakati wa kuzungumza juu ya mnyama hata wakati jinsia yake hujulikana:

 • "Pip, pip!" diris subite malgranda muso, kiu elkuris, kaj post ĝi venis ankoraŭ unu. - "Pip, pip!" Alisema ghafla panya mdogo ambaye alikimbia, na baadae alirudi mara moja.
 • Mi frapos vian ĉevalon sur la kapon tiel, ke ĝi falos senviva. - Nitawapiga farasi wako kichwani ili ianguke bila uzima(ife)

Katika matukio maalum wakati kunaweza kutokea kutokuelewana, mtu anaweza kutumia li au ŝi ikiwa ni wanyama.

1}Ĝi pia inaweza kuwakilisha kikundi cha maneno katika umoja kama: familia , jamaa , jeshi nk.

 • Hodiaŭ la problemo interesas la publikon, morgaŭ ĝi povas esti indiferenta pri ĝi. - Leo hii tatizo linahusu umma, kesho utakuwa haulijali.

  ĝi ya kwanza inawakilisha umma (watu kadhaa). ( ĝi ya pili ni tatizo.)

Ĝi} kwa kawaida huwakilisha kitu, mnyama na chochote kinachoelezea vizuri jambo. Tio hutumiwa kwa kuhusisha kitu ambacho haikionekani, kwa kuwakilisha sentensi nzima, au kwa jambo lisilojulikana (= jambo hili ):

 • — Ŝi forvojaĝis. — Jes, mi tion scias. = Jes, mi scias, ke ŝi forvojaĝis. - Alienda mbali.-ndiyo,nafahamu hivyo.=Nafahamu kwamba alienda mbali.

Ili

Ili ni wingi. Ili na ilia hutumiwa kwa kuzungumza juu ya mambo kadhaa au watu (isiyojumuisha msemaji wala msikilizaji). 1} Ili haionyeshi jinsia.

 • Kie estas la knaboj? Ili estas en la ĝardeno. - Wako wapi wavulana? Wako bustanini.
 • Kie estas la knabinoj? Ili ankaŭ estas en la ĝardeno. - Wasichana wako wapi? Wako pia bustanini.
 • Kie estas la tranĉiloj? Ili kuŝas sur la tablo. - Visu viko wapi? Viko mezani.
 • Donu al la birdoj akvon, ĉar ili volas trinki. - Wape ndege maji kwasababu wanataka kunywa.
 • Sinjoro Petro kaj lia edzino tre amas miajn infanojn; mi ankaŭ tre amas iliajn infanojn. - Bwana Petro na mke wake wanawapenda sana watoto wangu;Nami pia nawapenda watotot wao.

Katika lugha zingine, kiwakilishi ili hutumiwa mara kwa mara kwa watu wasiojulikana. Katika Kiesperanto mtu lazima atumie oni katika kesi hiyo.

Oni

Oni na onia ni viwakilishi vya kitu kisichojulikana ambavyo hutumiwa wakati wa kuzungumza juu ya mtu yeyote, watu kwa ujumla bila kutaja mtu yeyote hasa, pindi si lazima kumtambuwa. Oni kwa kawaida ni umoja lakini pia inaweza kuwa wingi. Oni haionyeshe jinsia:

 • En malbona vetero oni povas facile malvarmumi. - Katika hali ya hewa mbaya unaweza kushikwa na baridi.
 • Kiam oni estas riĉa (aŭ riĉaj), oni havas multajn amikojn. - Wakati uko tajiri unapata marafiki wengi.
 • Oni diras, ke la vero ĉiam venkas. - Wanasema kwamba ukweli siku zote hushinda.
 • Kun bruo oni malfermis la pordegon, kaj la kaleŝo enveturis en la korton. - Kwa sauti walifunguwa geti na behewa likaingia uani.
 • Oni tiel malhelpis al mi, ke mi malbonigis mian tutan laboron. - Hawakunisaidia hadi nikaaribu kazi yangu yote.
 • La malpura aero malsanigas onin. - Hewa chafu huleta magonjwa.
 • Kiam oni venas al tiu urbo, oni devas atenti pri la krimuloj. Ili kapablas ŝteli eĉ oniajn vestaĵojn. - Wakati mtu atakapokuja katika jiji hili, lazima awaangalie wahalifu. Wana uwezo wa kuiba hata nguo za mtu.
 • Ne kritiku onin, ĉar oni povas ankaŭ vin kritiki. - Usiteti mwengine, maana wanaweza kukuteta na wewe.

Katika maongezi ni maramachache unaweza kutana onin na onia. Kwa sababu ya uhaba wake baadhi ya watu wanaona aina hizi kuwa za ajabu na kuepuka kuzitumia, hata wakati zinaweza kuwa muhimu.

Si

Si na sia ni viwakilishi vya nafsi yatatu maalum ambavyo wakati kamili lazima kutumika badala ya viwakilishi vya nafsi yatatu vya kawaida. Si iko kwa umoja,kwa wingi kulingana na kile kinachowakilishwa. Si yenyewe haionyeshi jinsia.

Mara nyingi jambo hilo linaonekana kama kiima linaonekana na kazi nyingine katika sentensi moja. Ikiwa kiima ni mi, ni au vi (au ci), tunarudia tu kiwakilishi hicho hicho.

 • Mi lavas min. - Najisafisha mwenyewe.

  mi mbili ni mtu mmoja.

 • Mi vidas mian fraton. - Namuona kaka yangu.

  Minamiahuonyesha mtu mmoja.

 • Ni lavas nin. - Tunajisafisha wenyewe.

  Hizo nini watu wamoja.

 • Ni vidas niajn fratojn. - Tunawaona kaka zetu.

  Ninaniahuonyesha watu wamoja.

 • Vi lavas vin. - Mnajisafisha wenyewe.

  vi mbili ni watu wa wamoja

 • Vi vidas viajn fratojn. - Mnaona kaka zenu.

  Viandviahuonyesha watu wamoja.

Lakini kama kiima ni nafsi ya tatu (si msemaji wala msikilizaji), mtu lazima atumie si kwa jukumu jingine. Ikiwa, kwa mfano, unatumia li kwa kiima na kwenye kazi nyingine basi ni watu wawili tofauti. inafanana na ŝi, ĝi kaj ili:

 • Ŝi lavas ŝin. - anamsafisha.

  Mwanamke mmoja humuosha mwanamke mwingine.

 • Ŝi lavas sin. - Hujiosha mwenyewe.

  Mwanamke mmoja hujiosha mwili wake mwenyewe.Ŝi na sin zinaonyesha mtu huyo.

 • Ŝi vidas ŝian patrinon. - Anaona mama yake.

  Mwanamke mmoja huona mama wa mwanamke mwingine.

 • Ŝi vidas sian patrinon. - anaona mama yake.

  Mwanamke mmoja huona mama yake mzazi.

 • La virino serĉas ŝian filon. - Mwanamke anatazama kijana wake.

  Mwanamke anatazama kijana wa mawanamke mwingine.

 • La virino serĉas sian filon. - Mwanamke anatazama kijana wake.

  Mwanamke anatazama kijana wake binafsi.

 • Li lavas lin. - Anamuosha yeye.

  Mwanaume anamsafisha mawanaume mwingine.

 • Li lavas sin. - Anajiosha mwenyewe.

  Mwanaume huosha mwili wakebinafsi.Li nasin huonyesha mtu mmoja

 • Ĝi lavas ĝin. - Anamuosha.

  mnyama mmoja anamuosha mwingine mnyama(au kitu).

 • Ĝi lavas sin. - anajiosha yenyewe.

  Mnyama mmoja huosha mwili wake.Ĝinasin huonyesha mnyama mmoja.

 • La hundo ludas per sia pilko. - Mbwa hucheza nampira wake.

  Mbwa hucheza na mpira inaoumiliki yeye.

 • Ili lavas ilin. - Wanawaosha wao.

  kundi moja la watu au wanyama huosha kundi jingine.

 • Ili lavas sin. - hujiosha wao wenyewe.

  Kundi moja hujiosha miili yao.llisinhuonyesha kundi moja.

 • La naĝintoj ne trovas siajn vestaĵojn. - Waogeleaji hawapati nguo zao.

  Waogeleaji hawapati nguo zao binafsi.

 • Oni ne forgesas facile sian unuan amon. - Hauwezi kusahau kiurahisi mpenzi wako wa kwanza.

Sihaliwezi kuwa kiima

Si haiwezi kuwa yenyewe kiima au sehemu ya kiima, kwa sababu basi si ingejiwakilisha. Ata sia haiwezi kuwa sehemu ya kiima. Haiwezekani kusema: Si manĝas. Mi kaj si dancas. Petro kaj si fiŝkaptas. Mia kaj sia fratoj estas samklasanoj. Sia edzino estis kisata de li.Usiseme: Karlo kaj sia frato promenas en la parko. Ikiwa mtu anaweza kusema sentensi hiyo, angelenga kusema kwamba sia iwakilishe Karlo, lakini kiima sio Karlo, lakini Karlo kaj sia frato. Sema: Karlo kaj lia frato promenas en la parko. Hata hivyo mtu anaweza kutumia si, kwa kubadilisha sentensi hivi: Karlo kun sia frato promenas en la parko. Sasa kiima ni Karlo, na sia kwa usahihi inawakilisha Karlo. Maneno kun sia frato [pamoja na ndugu yake] si sehemu ya kiima, lakini kun -adject.

Si katika hali kutendewa

Si na sia inawakilisha kiima cha Sarufi . Hii pia inatumika kwenye hali ya kutendewa, ingawa kiima cha sarufi sio mtendaji katika aina hiyo sentensi:

 • Ŝi estas amata de siaj instruistinoj. - Anapendwa na walimu wake.
 • Karlo estis akompanata de Petro al sia domo. = ...al la domo de Karlo. - Karlo alikuwa akisindikizwa na Petro nyumbani kwake. = ... nyumbani kwa Karlo.
 • Karlo estis akompanata de Petro al lia domo. = ...al la domo de Petro. - Karlo alikuwa akisindikizwa na Petro nyumbani kwake.=nyumbani kwa Petro.
 • Li sendas leteron al sia kuzo.Letero estas sendata de li al lia (propra) kuzo. - Alituma barua kwa binamu yake.→barua ilitumwa na yeye kwa binamu yake binafsi.

  Kwa sentensi isiyo ya kawaida huwezi kusema al siazo , kwa sababu basi tutazungumzia barua ya binamu.

kishazi tegemezi

Prediketo kishazi tegemezi kina kiima chake. Ikiwa unatumia si(a) katika kishazi tegemezi mara zote iwakilishe kiima, kamwe si kiima cha kishazi huru:

 • Elizabeto rigardis la viron, kiu kombis al si la harojn. - Elizabeth alitazama mwanaume ambaye alitana nywele zake.

  Mtu huyu alitana nywele zake (sio za Elizabeth). Si inawakilisha kiima cha kombis, yaani kiu (na kiu inawakilisha mwanaume).

 • Karlo kaj Petro diris, ke la infanoj jam vestis sin. - Karlo na Petro walisema kwamba watoto wamesha jivika wao wenyewe.

  Watoto walijivika wao wemyewe.(hawkuvikwa na Karlo na Peter).

 • Li vidis, ke la hundo ludas per sia pilko. - Aliona kwamba mbwa anacheza na mpira wake.

  Mbwa anamiliki mpira wake(kiima cha kishazi tegemezi).

 • Abimeleĥ, la reĝo de la Filiŝtoj, rigardis tra la fenestro, kaj vidis, ke Isaak amuziĝas kun sia edzino Rebeka. - Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, akatazama nje ya dirisha na kuona kwamba Isaka anaburudika na na mkewe Rebecca.

  Rebecca ni mke wa Isaka (kiima chaamuziĝas, si wa Abimeleki (kiima cha vidis, kama angekuwa mke wa Abimeleki, mtu angesema lia edzino{ 2}.

 • Mia avo diris, ke li tre amis sian patrinon. - Babu yangu alisema kwamba alikuwa alimpenda mama yake sana.

  Sian inawakilisha kiima cha amis, li inaweza kutaja mia avo, lakini inaweza pia kuwa mtu mwingine.

Si haiwezi kuwa yenyewe kiima. Pia haiwezekani kuitumia si kama kiima cha kishazi tegemezi, wala kama sehemu ya kiima cha kishazi tegemezi kwa lengo la kufanya si iwakilishe kiima cha kishazi huru. Huwezi kusema: Karlo diris, ke si venos morgaŭ. Wala: Karlo diris, ke sia frato venos morgaŭ. Si katika kishazi tegemezi daima kinamaanisha kiima cha kishazi tegemezi. Mtu lazima aseme: Karlo diris, ke li venos... / ke lia frato venos... Pia huwezi kusema: Ŝi sentis, ke pluvas sur sin. Lazima useme: Ŝi sentis, ke pluvas sur ŝin.

Participle yenye A mwishoni kama kishazi tegemezi:

 • Li ekvidis la anĝelon de la Eternulo, starantan sur la vojo kun elingigita glavo en sia mano. - Aliona ghafla malaika wa Bwana amesimama barabarani na akishuka na upanga mkonpni mwake.

  Malaika alikuwa amesimama na upanga mkononi mwake.

 • Karlo promenis kun virino vestita per sia plej bela vesto. - Karlo katembea na mwanamkea aliyekuwa amevaa nguo zake nzuri.

  Alikuwa amevaa nguo zake nzuri.

Pia maelezo ya kulinganisha yaliyoanzwa na kiel au ol ni kama kishazi tegemezi. Si katika maneno haya ya kulinganisha iwakilishe kiima cha la kitenzi ambacho hakieleweki vizuri:

 • Ŝi amas lin kiel sin mem. - Alimpenda kama yeye mwenyewe.

  Alimpenda yeye kama alivyojipenda mwenyewe.

 • Ŝi estas tiel saĝa kiel ŝia fratino. - Ni mwenye busara kama dada yake.

  Na dada yake pia ana busara.

 • Li punis ilin same kiel siajn fratojn. - aliwaadhibu kama kaka zake.

  Aliwaadhibu pia kaka zake.

 • Ŝi amas lin pli ol sin mem. - Alimpenda yeye kuliko alivyojipenda.

  Alimpenda yeye kuliko alivyojipenda yeye mwenyewe.

 • Li estas pli aĝa ol lia frato. - Ana mriu mkubwa kuliko kaka yake.

  Kaka yake ni mkubwa laikni wa chini kwa huyu.

Wasifu tatanisho iliyowekwa baadae au nyongezo ya nomino inaweza kuhesabiwa kama kishazi tegemezi ambacho maana yake haisikiki vizuri. Kisha si inaweza kuwakilisha kiima cha kitenzi ambacho hakisikiki vizuri. Kishazi tegemezi daima linafanana na nomino la awali. Kwa aina hizi za sentensi matumizi hata hivyo yako tofauti:

 • Ili vizitis muzeon faman pro siaj belaj pentraĵoj. = ...muzeon, kiu estas fama pro siaj belaj pentraĵoj. - Walitembelea makumbusho maarufu kwa uchoraji wake mzuri. = ... makumbusho ambayo inajulikana kwa uchoraji wake mzuri.

  Sanamu ni cha makumbusho.

 • Picasso vizitis muzeon faman pro liaj pentraĵoj. = ...muzeon, kiu estas fama pro liaj pentraĵoj. - Picasso alitembelea makumbusho maarufu kwa michoro yake. = ... makumbusho ambayo inajulikana kwa uchoraji wake.

  Sanamu ni ya Picasso.

 • Ŝi vidis soldaton kun sia pafilo en la mano. = ...soldaton, kiu staris kun sia pafilo en la mano. - Alimwona askari akiwa na bunduki yake mkononi. = ... askari aliyesimama na bunduki yake mkononi.

Infinitive

Wakati si inatumiwa pamoja na mfumo wa infinitive, ksi inawakilisha kiima chenye maana ya infinitive. Katika hali nyingi hii kiima hicho ni sawa na kiima cha prediketo, lakini si kila siku:

 • Ĉiu homo devas zorgi pri si mem. - Kila mtu lazima ajitazame yeye mwenyewe.

  Si inawakilisha kiima cha zorgi .Kinafanana na kiima cha devas.

 • La sinjoro ordonis al la servisto vesti sin. - Bwana aliamuru mtumishi ajivike mwenyewe.

  Kiima cha vesti ni la servisto. Sin inawakilisha mtumishi.

 • La sinjoro ordonis al la servisto vesti lin. - Bwana aliamuru mtumishi amvike.

  Mtumishi hakuvaa, asijiviki, bali mtu mwingine, inawezekana kuwa ni huyo bwana.

Ikiwa kiima chenye maana cha infinitive hakipo katika sentensi, na kikiwa sio muhimu, basi kawaida unaachia si iwakilishe kiima cha prediketo:

 • La reĝo sendis voki sian kuraciston. - Mfalme aliagiza waite mganga wake.

  Kiima cha voki hakipo katika sentensi na sio muhimu. Sia, kwa hiyo, inaweza kumwakilisha mfalme. Tunachukulia sendis voki kama kitenzi kimoja na kiima kimoja tu, mfalme.

 • La reĝo sendis la serviston voki lian kuraciston. - Mfalme alimtuma mtumishi kumwita Mganga wake.

  Hapa kiima cha voki (mtumishi) kipo. Ikiwa mtu angeweza kusema sian kuraciston, basi mtumishi angepaswa kumwita daktari wake binafsi 9mganga wa mtumishi), si daktari wa mfalme.

Nomino fanyakazi

Ikiwa nomino inafanya kazi hadharani, na kama kiima chake kipo si inapaswa kawaida kuwakilisha kiima hicho. Hata hivyo, kanuni haijafanywa:

 • Petro pacience aŭskultis la plendadon de Karlo pri ĉiuj siaj problemoj. - Petro alisikiliza kwa subira malalamiko ya Karlo juu ya matatizo yake yote.

  Karlo alilalamika kuhusu matatizo yake. Matatizo ni ya Karlo(kiima cha plendado), na sio cha Petro (kiima cha aŭskultis).

Wakati sia imewekwa kabla ya nomino tendaji kama tambulisho, daima inawakilisha kiima cha prediketo:

 • Karlo rakontis al Eva pri sia vojaĝo al Azio. - Karlo alimwambia Eva kuhusu safari yake ya Asia.

  Karlo alisafiri Asia.

 • Karlo demandis al Eva pri ŝia vojaĝo al Eŭropo. - Karlo alimuuliza Eva kuhusu safari yake ya Ulaya.

  Eva alisafiri Ulaya.

Si(a) katika maelezo yaliyo maalum

Katika baadhi ya maelezo maalum si(a) hayatii sheria za kawaida:

 • siatempe = "wakati huo, wakati sahihi, kwa fursa". Wakati siatempe ina maana hii maalum, tunasema mara nyingi siatempe bila kujali kiima: Nilitaka kwenye muda mwafaka nipendekeze sheria. Kipindi hicho nitaipa nchi yako mvua wakati mzuri.
 • Nomino + en si = "kama ilivyo". Wakati wa kueleza maana hii maalum tunatumia si hata kama kitu kinachozungumziwa si kiima: Se oni rigardas la aferon en si, oni vidas...= Ukiangalia jambo hilo kama lilivyo... .
Kurudi juu