Kwa maudhui

Apposition ni maelezo inayowekwa baada ya kipengele cha sentensi. Inaonyesha kitu kimoja kwa maneno mengine. Apposition kwa njia fulani inaelezea maneno ya awali, lakini hata hivyo ni maneno yake. Katika maongezi, unatambua apposition kwa mapumziko madogomadogo kabla na baadae. Katika maandishi mara nyingi wanaweka mkato.

Apposition ina jukumu sawa na kifungu kilichotangulia. Ikiwa kifungu cha awali ina mwisho wa accusative N, apposition inapaswa pia inapata mwisho huyo:

 • Karlo, nia prezidanto, prezentis Petron, la novan sekretarion. - Carlos, rais wetu, alitambulisha Petro, katibu mpya.

  Karlo na nia prezidanto ni viima, wao ni mtu mmoja. NaPedro na katibu mpya ni shamrisho, kwa sababu ni sawa.

 • Tie mi renkontis Vilĉjon, mian edzon. - Huko nilikutana na Vilĉjon, mume wangu.
 • La diablo lin prenu, la sentaŭgulon! - Shetani amchukue yeye, uyo mgeni!
 • La koko, trumpetisto de l' mateno, per sia laŭta, forta, hela voĉo el dormo vekas dion de la tago. - Jogoo, tarumbeta ya asubuhi, kwa sauti yake kubwa, yenye nguvu, sauti nzuri huamsha mungu wa siku kutoka usingizi wake.
 • Li prelegis pri Hitlero, la fondinto de la naziismo. - Alitoa hotuba kuhusu Hitler, mwanzilishi wa nazism.

  Wanaweza kusema:...pri Hitlero, pri la fondinto...

 • Ni esprimas nian koran dankon al sinjoro Schleyer, la unua kaj plej energia pioniro de la ideo de neŭtrala lingvo internacia. - Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa bwana Schleyer, mwanzilishi wa kwanza na mwenye nguvu sana wa wazo la lugha ya kimataifa isiyokuwa na upande.

  Wanaweza kusema:...al sinjoro Schleyer, al la unua kaj plej energia pioniro...

Wakati mwingine wanatanguliza apposition na nome (yaani), tio estas (hiyo ni), au maneno kama hayo:

 • Mi renkontis mian malamikon, nome la mortiginton de mia patro. - Nilikutana na adui yangu, yaani muuwaji wa babangu.
 • Hodiaŭ mi ricevis duoblan pagon, tio estas cent dolarojn. - Leo nimepata malipo mara mbili ya, hizo ni dola mia moja.

  Ufupisho wa:Tio estas: mi ricevis cent dolarojn. (hiyo ni: nilipata dola mia moja.)

Usichanganye apposition na nominative. Nominative yaweza kufanana na appositio, lakini nominative haikubali mwisho N au kingine kiashiria kingine. Linganisha sentensi zifuatazo:

 • Iuj asertis, ke ili vidis eĉ profesoron, Paŭlon Jenkins. - Wamoja walikubali kwamba wameona profesa, Paulo Jenkins.

  Cha kushangaza ni kwamba wote wameona profesa. Kisha imeongezwa kuwa wameona tu Paulo Jenkins. Paul Jenkins ni apposition.

 • Iuj asertis, ke ili vidis eĉ profesoron Paŭlo Jenkins. - Wengine walisema kwamba walimuona hata profesa Paul Jenkins.

  Mshangao ni kwamba wameona Paulo Jenkins (ambaye ni profesa). Paulo Jenkins ni nominative ya profesa. Profesa Paulo Jenkins = ule profesa aitwaye Paulo Jenkins.

Usichange apposition na jukumu vocative, ambayo haina kiashiria: Sidigu vin, sinjoro! (Kaa chini, bwana!) Vin na sinjoro ni mtu mmoja, lakini vin ni shamrisho, na sinjoro vocative.

Apposition ĉiu(j) , ambaŭ au ĉio

Ĉiu(j), ambaŭ na ĉio inaweza kuwa apposition ya kueleza jina au kiwakilishi nafsi. Ikiwa nomino au kiwakilishi vina mwisho N, basi apposition lazima iwe na mwisho huyo (isipokuwa ambaŭ ambayo haiwezi kuwa na mwisho N). Apposition za aina hii hazisimami moja kwa moja baada ya kifungu cha kwanza, lakini mara nyingi baadae kidogo katika sentensi:

 • Ni ĉiuj legas. = Ni legas. Ĉiuj (el ni) legas. - Sisi sote tusoma.= tunasoma. Sote(miongoni mwetu) tunasoma.
 • Ili ĉiuj sidas silente kaj skribas. = Ili sidas. Ĉiuj (el ili) sidas. - Wote wameketi kimya na kuandika. = Wameketi. Wote (wao) wameketi.
 • Ŝi vidis, kiel la cikonioj forflugis, ĉiu aparte. = La cikonioj forflugis. Ĉiu unuopa cikonio forflugis aparte. - Aliona jinsi korongo waliruka, kila mmoja. = Korongo waliruka. Kila korongo moja moja aliruka.
 • La kolonoj havis ĉiu la alton de dek ok ulnoj. Ĉiu unuopa kolono estis tiel alta. - Kila nguzo ilikuwa na urefu wa mikono kumi na nane. Kila nguzo moja ilikuwa ndefu.
 • Vin ĉiujn mi kore salutas. = Mi salutas vin. Mi salutas ĉiujn (el vi). - Ninyi nyote nawapa salamu za dhati.= Nawasalimu ninyi. Nawasalimu wote (nyinyi wote).
 • Ili ambaŭ estis bonaj homoj. = Ili estis bonaj homoj. Ambaŭ (el ili) estis bonaj homoj. - Wote wawili walikuwa watu wema.= Wao walikuwa watu wema. Wote wawili (wao) walikuwa watu wema.
 • Tio estas ĉio tre bona. = Tio estas tre bona. Ĉio (el tio) estas tre bona. - Hiyo yote ni nzuri sana,= Hiyo ni nzuri sana. Kila kitu (kutoka miongoni mwao) ni kizuri sana.

Muungano wa maandishi

Muundo maalum wa apposition ni muungano. Katika muungano maneno kadhaa (mara nyingi naneno mawili) ya aina moja yanajumuika kueleza kitu maalum. Maneno tofauti katika muungano yanakuwa karibu neno moja. Wanayatamka mara moja bila kupumzika, ila wanatumia kistariungio. Hata hivyo, sio muungano halisi. Kisarufi tunayachukulia (kawaida) kama maneno tofauti:

 • Pluraj ŝtatoj-membroj informis pri sia preteco ampleksigi la instruadon de Esperanto. = ...ŝtatoj, kiuj estas membroj [de UNESKO]... - Nchi nyingi wanachama wamejulisha kuwa ziko tayari kupanua mafundisho ya Kiesperanto. = ... Mataifa ambayo ni wanachama [wa UNESCO] ...

  Ikiwa ŝtatoj, na membroj yana mwisho J kwa sababu ni maneno mawili tofauti.

 • La Franca flago estas blua-blanka-ruĝa. - Bendera ya Ufaransa ni bluu-nyeupe-nyekundu.

  Mmoja anaweza pia kusema blua, blanka kaj ruĝa , lakini fomu ya muungano huonyesha kwamba tunazungumzia kuhusu mchanganyiko wa rangi ya uhakika iliyotolewa kama kitengo kimoja.

 • La fotoj ne estis koloraj, sed nigraj-blankaj. - Picha hazikuwa na rangi, lakini nyeusi-nyeupe.

  Unaweza pia kusema nigraj kaj blankaj, lakini nigraj-blankaj inasisitiza kwa kiasi kikubwa tofauti kwa koloraj. Ni aina fulani ya picha.

 • Kio estos, tio estos, mi provos trafe-maltrafe. = ...mi provos, ĉu trafe, ĉu maltrafe, laŭ ŝanco. - Lenye litakuwa litakuwa, nitajaribu homba-homboka. =...nitajaribu, nipate au nikose kulingana na bahati.
 • Vole-ne-vole li devis konsenti. = Ĉu vole, ĉu ne-vole, li devis konsenti. - Atake asitake alilazimika kukubali. = Ikiwa kwa hiari, au bila hiari, alilazimika kukubali.
 • Pli-malpli unu horon poste Marta eniris en sian ĉambreton en la mansardo. = Proksimume unu horon poste... - Kidogo lisaa limoja baadae Martha aliingia ndani ya chumba chake kidogo kwenye dari. = Karibu saa moja baadae ...

  Wakati mwingine unaweza kusema pia pli aŭ malpli, lakini hii haina maana ya proksimume. (karibu)

Apposition ya kuonyesha maoni.

Wakati mwingine tunatumia maneno kama apposition ambayo hayaonyeshi kitu kimoja, lakini yanayoongeza maelezo kuhusu jambo hilo. Mara nyingi ni mahali ambapo jambo lipo, au linatoka. Maoni kama apposition kamwe haikubali mwisho N. Mtu anaweza kutazama apposition kama vishazi tegemezi vifupi:

 • Prelegis interalie profesoro Kiselman, Svedujo. = ...Kiselman, kiu venas el Svedujo. - Profesa Kiselman, Sweden, alitoa hotuba. = ... Kiselman, anatoka Sweden.

  Unaweza pia kusema: ...Kiselman el Svedujo.

 • Ni vizitis Tokion, Japanujo. = ...Tokion, kiu troviĝas en Japanujo. - Tulikutembelea Tokyo, Japani. = ... Tokyo ambayo hupatikana huko Japan.

  Au: ...Tokion en Japanujo.

Kurudi juu