Nambari
Nambri ni maneno ambayo yanaonyesha idadi. Kuna nambari kumi na tatu katika Kiesperanto:
- nul
- 0
- unu
- 1
- du
- 2
- tri
- 3
- kvar
- 4
- kvin
- 5
- ses
- 6
- sep
- 7
- ok
- 8
- naŭ
- 9
- dek
- 10
- cent
- 100
- mil
- 1000
Idadi zingine zinaonyeshwa kwa kuchanganya nambari. Kwanza, wnsema ni maelfu ngapi, kisha ni mamia ngapi, alafu ni makumi ngapi, na hatimaye ni mamoja ngapi:
- 11
- dek unu
- 12
- dek du
- 13
- dek tri
- 14
- dek kvar
- 15
- dek kvin
- 16
- dek ses
- 17
- dek sep
- 18
- dek ok
- 19
- dek naŭ
- 20
- dudek
- 21
- dudek unu
- 22
- dudek du
- 23
- dudek tri
- 30
- tridek
- 40
- kvardek
- 50
- kvindek
- 60
- sesdek
- 70
- sepdek
- 80
- okdek
- 90
- naŭdek
- 100
- cent
- 101
- cent unu
- 110
- cent dek
- 111
- cent dek unu
- 200
- ducent
- 232
- ducent tridek du
- 300
- tricent
- 400
- kvarcent
- 500
- kvincent
- 600
- sescent
- 700
- sepcent
- 800
- okcent
- 900
- naŭcent
- 1000
- mil
- 1001
- mil unu
- 1011
- mil dek unu
- 1111
- mil cent dek unu
- 1234
- mil ducent tridek kvar
- 2000
- du mil
- 2678
- du mil sescent sepdek ok
- 3000
- tri mil
- 4000
- kvar mil
- 5000
- kvin mil
- 6000
- ses mil
- 7000
- sep mil
- 8000
- ok mil
- 9000
- naŭ mil
- 10000
- dek mil
- 11000
- dek unu mil
- 12000
- dek du mil
- 20000
- dudek mil
- 30000
- tridek mil
- 42000
- kvardek du mil
- 999000
- naŭcent naŭdek naŭ mil
- 999999
- naŭcent naŭdek naŭ mil naŭcent naŭdek naŭ
Makumi na mamia vinaandikwa kwa pamoja (na kutamkwa) kama neno moja moja: dudek, tridek, ducent, tricent n.k. Kila kitu kingine kinapaswa kuandikwa kama maneno tofauti, pia na maelfu.
Makumi na mamia hupokea kama maneno mengine lafudhi katika vokali yapilimwisho: dUdek, trIdek, dUcent, trIcent. Kila kitu kingine kinasemwa kama maneno tofauti: dEk dU, dEk trI, cEnt dU, cEnt trI, cEnt dEk dU, dU mIl, trI mIl, dU mIl dEk dU.
Ikiwa kwenye maneno ya kimsingi ya msingi panaundwa mkusanyiko wa maneno, kwa mfano majina au vivumishi vya idadi, hata hivyo, mtu anaweza au anaweza kuyaunga, pengine kwa vistariungio.
Nul awali ilikuwa jina: Nulo (jina la nmbari). Lakini pia hutumiwa kama nambari kwa muda mrefu, kwa mfano: 0,5 = nul komo kvin (au nulo komo kvin).
Mara kwa mara, fomu iliyofupishwa nul'inaweza kutumika badala ya unu.
Matumizi ya nambari
Mara nyingi nambari huonekana kama wsifu. Nambari kipindi hicho hazichukuwi mwisho N na J:
- Mi havas nur unu buŝon, sed mi havas du orelojn. - Nina mdomo mmoja tu, lakini nina masikio mawili.
- Li faris ĉion per la dek fingroj de siaj manoj. - Alifanya kila kitu kwa vidole kumi vya mikono ya mikono yake.
- Li havas dek unu infanojn. - Ana watoto kumi na mmoja.
- Sesdek minutoj faras unu horon, kaj unu minuto konsistas el sesdek sekundoj. - Dakika sitini hukamilisha saa moja, na dakika moja ni sekunde sitini.
Wakati mwingine jina hilo huondolewa (linaeleweka kwa mbali):
- Nu, se vi ne havas mil [rublojn], mi petas cent rublojn. - Naam, kama hauna ruble elfu, nitakuomba ruble mia
- Kiun el la tri [aferoj/personoj] vi elektas? - Ipi miongoni mwa [vitu/watu] watatu unachagua?
Nul (sufuri) huonekana kama wasifu wa nambari tu kabla ya mamoja ya kipimo:
-
La frostpunkto de akvo estas nul gradoj ĉe norma atmosfera premo. - Maji yanagandana kwenye digrii sufuri kwenye kanieneo angahewa ya kawaida.
Kwa kawaida tunaandika 0 gradoj, lakini tutatamka kama nul gradoj .
- Ilia fina rezulto estis nul poentoj. - Hitimisho ya matokeo ilikuwa pointi sufuri.
Katika matukio mengine kawaida neniu hutumiwa: Mi havas neniun malamikon.
Nambari zinaweza pia kuonekana zenyewe katika jukumu mbaimbali za sentensi. Mara nyingi majukuma yao ni kama nomino. Mwisho J au N haitumiwi kamwe:
- Kvin kaj sep faras dek du. - Tano kujumlisha saba sawa sawa na kumi na mbili.
- Tridek kaj kvardek kvin faras sepdek kvin. - Thelathini kujumlisha arobaini na tano sawa sawa na Sabini na tano.
- Ilia nombro estas kvardek tri mil sepcent tridek. - Idadi yao ni arobaini na tatu elfu mia saba na thelathini.
- Divido per nul ne estas permesita. - Kugawanyika kwa sifuri hakuruhusiwi.
- Tri estas duono de ses. - Tatu ni nusu ya Sita.
- Sep estas sankta nombro. - Saba ni namba takatifu.
-
Mi legis numeron 2 de la jaro 1990. - Nimesoma namba mbili kutoka mwaka 1990.
Ni namba ya gazeti.
- Ni loĝas en ĉambro tricent tridek tri en tiu hotelo. - Tunaishi katika chumba cha mia tatu na thelathini na tatu katika hoteli hiyo.
Linapokuja nambari, mtu anaweza pia kutumia namba ngazi: la dua numero, la jaro 1990-a, la tricent-tridek-tria ĉambro. Lakini kunaweza kutofautiana kati ya oda na namba. Kwa mfano: yanne inamaanisha kulikuwa na wengine watatu hapo awali kwenye oda, wakati namba nne inamaanisha kwamba jambo hilo lina nambari 4 kama aina ya "jina". Kwa mfano Hoteli mara nyingi hawana idadi, na ndiyo sababu. Chumba mia si lazima chumba chamia. Na kama unasimama mwishoni mwa barabara, unaweza kusema kwamba nyumba namba moja sio nyumba ya kwanza, lakini ya mwisho.
Matumizi maalum ya moja
Maana ya msingi ya unu ni namba. Matumizi haya yalielezwa hapa pamoja na nambari nyingine. Lakini unu pia ina maana na matumizi maalum. Unu inaweza kueleza, ufananaji, ubinafsi na utambulisho:
- La loĝantoj de unu regno estas samregnanoj, la loĝantoj de unu urbo estas samurbanoj, la konfesantoj de unu religio estas samreligianoj. = La loĝantoj de unu sama regno... - Wakazi wa ufalme umoja ni wanaufalme wamoja, wakazi wa mji mmoja ni wanamji wamoja, waumini wa dini moja ni wanadini wamoja. = Wakazi wa ufalme umoja ...
-
Ŝin trafis unu malfeliĉo post la alia. - Alipata na tabu baada ya mwingine.
Hapa unu inasisitiza ubinafsi wa kila tabu. Kwa maana hiyo unu mara nyingi hushirikiana na alia.
-
En unu tago, kiam ŝi estis apud tiu fonto, venis al ŝi malriĉa virino. - Siku moja alipokuwa karibu na chemchemi hiyo, mwanamke maskini alikuja kwake.
Ni siku inayojulikana kwa msemaji, lakini si kwa msikilizaji. Katika matumizi hayo unu ni nusu kibainishi wazi .
1}Unu pia hutumiwa kwa kibinafsi bila jina la baadae. Mara nyingi inawezekana kusema kwamba jina linasikika kidogo, lakini wakati mwingine kuongeza jina litaweza tu lingekera. Kisha unu hutumiwa kama kiwakilishi:
- Ŝi estis unu el la plej belaj knabinoj, kiujn oni povis trovi. - Alikuwa mmoja wa wasichana waliovutia zaidi ambao wangeweza kupatikana.
- Unu babilis, alia kantis. - Mmoja alizungumza, mwingine aliimba.
Wakati yabinafsi au yakiwakilishi (wakati mwingine pekee) unu hutumiwa kwa watu kadhaa, hupokea mwisho J:
- El ŝiaj multaj infanoj unuj estas bonaj kaj aliaj estas malbonaj. - Kati ya watoto wake wamoja ni wazuri na wengine ni wabaya.
- Dum unuj artikoloj alportas al nia afero rondon da novaj amikoj, multaj aliaj, skribitaj nelerte, tute perdiĝas sen rezultato. - Kipindi makala moja hutuletea marafiki wapya kwenye mambo yetu, wengine wengi ambao hawakuandikwa vizuri, hawapatikani kabisa bila matokeo.
- Unuj [studentoj] kun gaja rideto sur la buŝo, aliaj meditante, aliaj en vigla interparolado, unuope aŭ duope forlasas la universitatan korton. - [Wanafunzi] wamoja na tabasamu ya furaha juu kwenye midomo yao, wengine wakitafakari, wengine katika mazungumzo ya kazi, mmoja mmoja au wawili wawili wanatoka nje ya chuo.
Fomu unu haiwezi kupokea mwisho N. Hii ni kanuni ya msingi ambayo inatumika kila wakati, ikiwa unu inaonyesha namba, ingawa ikionyesha ubinafsi, iwe ya pekee: Unu mi renkontis en Londono, alian en Parizo. Usitumie fomu unun. Lakini fomu unuj inaweza kupata mwisho N, kwa kuwa unuj haiwezi kuwa namba sasi. Daima inaonyesha ubinafsi au upekee. Fomu unujn inahitajika mara chache sana: Unujn mi renkontis en Londono, aliajn en Parizo.
Kanuni inayokataza unun, lakini inaruhusu unujn, ni ya ajabu kutoka kwa mtazamo wa mantiki. Lakini ni nzuri sana kutoka kwa mtazamo wa matumizi. Katika matumizi ya namba, ya kipekee na ya kibinafsi ya unu haitafatishwi sana. Kuna vikwazo vingi, na hivyo kanuni rahisi kwamba unu isiwe na mwisho N kabisa ni inajulikana. Si lazima kuaza kila wakati, ikiwa unu inaonyesha namba, upekee au ubinafsi. Unuj daima huonyesha ubinafsi au upekee, na kwa hiyo hakuna tatizo la kutumia baada yake mwisho N, ikiwa jukumu ndani ya sentensi linahitajika.
Usichanganishe ubinafsi moja unu na correlative iu . Unu ya ubinafsi inaonyesha kwamba msemaji anajua vizuri mtu anayezungumza (kipindi msikilizaji labda hajui). Iu inaonyesha kwamba utambulisho wa mtu anayesemwa haijulikani au haiko wazi, au kwamba utambulisho si muhimu:
-
Loĝas ĉi tie unu el viaj amikoj. - Kuna mmoja wa marafiki zako anaishi pale.
Msemaji anajua nani katika marafiki anaishi hapa pale.
-
Loĝas ĉi tie iu el viaj amikoj. - Baadhi ya marafiki zako wanaishi hapa.
Msemaji (pengine) hajui ni marafiki gani wanaoishi hapa.
Mara nyingi mtu anaweza kutumia iu badala ya unu, wakati si muhimu kuonyesha kama mtu anajulikana kwa msemaji. Lakini unu inaonyesha vizuri zaidi. Inaonyesha kwamba msemaji anajua utambulisho.
Kivumishicerta ina wakati mwingine maana sawa na unu ya ubinafsi, lakini certa ina nguvu zaidi. Inasisitiza kuwa kitu kinajulikana kwa msemaji (lakini sio kwa msikilizaji): certaj okazoj multe da saĝo estas pli malbona, ol se oni ĝin tute ne havus. Hieraŭ vizitis min certa sinjorino Schmidt.
Matumizi mbalimbali ya unu inaonekana ya ajabu kwa baadhi ya watu, kati ya maneno mengine kwa sababu vitabu havielezei mara kwa mara. Kwa hiyo wengi wanapendelea kutumia unu tu kwa jukumu la namba tu, na wanapendelea kwa maana nyingine maneno iu(j), kelka(j) na certa(j)}. Hii ni upungufu wa lugha, kwa kuwa maneno haya yote yanaonyesha maana tofauti, na maana yote vinahitajika.
Unu... la alia
Unu ya kiwakilishi ni sehemu ya msemo unu ... (la) alia ambayo inasaidia kunyesha ubadilishaji. Unu ... (la) alia inawakilisha sentensi nzima iliyofupishwa. Unu kawaida kiima cha sentensi kamili, na (la) alia ni shamrisho au ina jukumu jingine kinyume na kiima:
-
Tiuj gejunuloj amas unu la alian. → Tiuj gejunuloj amas. Unu amas la alian. - Hawa vijana hupendana. → Vijana hawa wanapenda. Mtu anapenda mwenzake.
Kila mmoja wao anapenda kila mmoja wao.
-
Ili donis florojn unu al alia. → Ili donis florojn. Unu donis florojn al alia. - Walipana maua. →Walitoa maua. Mmoja alimpa maua mwingine.
Kila mmoja alitoa maua kwa mwingine.
-
Li kunigis kvin tapiŝojn unu kun la alia. - Alifunga mazulia matano moja kwa moja. [Kutoka 36:10]
Aliweka pamoja zulia kwa lingine.
Unaweza karibuni kila mara kutumia unu ... (la)alia bila mwisho J. Ikiwa ni lazima, mwisho J unaweza kuongezwa kwa alia na pia La junaj knabinoj kaj junuloj ĉe la lageto babilas unuj kun la aliaj.unuLa registaroj ĵetas la homojn unujn kontraŭ la aliajn. = La registaroj ĵetas unujn homojn kontraŭ la aliajn homojn. kulingana na maana inayolengwa: La junaj knabinoj kaj junuloj ĉe la lageto babilas unuj kun la aliaj. Baadhi yao wanazungumza na wengine wao. Wakati mwingine fomu unujn inapaswa kutumika: La registaroj ĵetas la homojn unujn kontraŭ la aliajn. = La registaroj ĵetas unujn homojn kontraŭ la aliajn homojn.
Badala ya unu ... la alia (mmoja kwa mwingine), neno reciproke linaweza kutumiwa pamoja na si au kiwakilishi kingine: {3 } reciproke pia inaweza kutumika pamoja na unu ... la alia ili kusisitiza ubadilishji: Vi ne estas reciproke egalaj unu al la alia en la regiono de la spirito. Neno inter pia linaweza kutumika kama kiambishi kwa kitenzi, mara kwa mara na si au kiwakilishi kingine, au msemo inter si (kati ya/kati yao) (inter ni (kati yetu), }inter vi (miongoni mwenu)), ambayo mara zote inamaanisha unu kun alia (kwa pamoja) au kitu kama hicho: Ili sin interakuzas. = Ili akuzas unu la alian. Ili interparolas. = Ili parolas unu kun la alia. Ili estis tre amikaj inter si.Usitumie kmwe si pamoja na unu ... la alia. Usiseme: Ili amas sin unu la alian. Sema tu: Ili amas unu la alian.
Nambari ya majina
Maneno ya nambari na kiambishi kiambishi tamati ON huonyesha nambari za sehemu:
- duono = 1/2
- triono = 1/3
- dekono = 1/10
- dekduono = 1/12
- centono = 1/100
- milono = 1/1000
Namba ya juu kuliko 999999 huelezewa kwa kutumia nambari za majina:
- miliono
- 1.000.000(Sifuri sita)
- miliardo
- 1.000.000.000(=Sifuri tisa)
- biliono
- 1.000.000.000.000(Sifuri kumi na mbili)
- triliono
- {1]Sifuri kumi na nane)
Lugha zingine, kwa mfano Kiingereza na Kirusi, hutoa thamani nyingine kwa maneno ya nambari yenye mfumo mmoja kama biliono (bilioni) na triliono (trilioni). Maneno ya Kiesperanto lazima iwe na maana tu zilizoonyeshwa hapo juu, na hakuna zingine. Pia kuna idadi kubwa zaidi ya maneno ya aina hii, lakini hutumiwa mara kwa mara sana.
Namba za majina hupokea mwisho J na N kulingana na sheria sawa na majina mengine:
- Kiam vi havos rikolton, vi donos kvinonon al Faraono. - Wakati una mavuno, utampa Farao sehemu ya tano.
- Mi ricevis dudek kvin centonojn. - Nilipokea sehemu ya mia ya ishirini na tano.
- Ŝi havas pli ol dek milionojn. - Ana zaidi kuliko Milioni kumi.
- La malprofito atingis sumon de kvardek sep miliardoj. - Hasara ilifikia jumla ya bilioni arobaini na saba.
Nambari ya maneno katika fomu ya jina haiwezi kuelezea moja kwa moja nomino, ila hutumika pamoja na kihusishi da:
- Li havas du miliardojn da dolaroj. - Ana bilioni mbili za dola za kimarekani.
- Ŝi vidis pli ol dek milionojn da homoj. - Aliona zaidi ya watu milioni kumi.
Neno la ON- na mwisho O linahitaji msaada wa vihusishi: Unu tago estas tricent-sesdek-kvinono aŭ tricent-sesdek-sesono de jaro.
Namba pia zinaweza kuwa kama nomino ukiongeza mwisho-O.katika muundo huu, inaonyesha uhuusiano wa kitu na namba, au kundi na idadi hiyo ya vitu. Kabla ya mwisho O kila siku zinaandikwa na nambari. Kwa kuweka wazi unweza kutumia kistariungio pale ambapo kuna nafasi:
- unu → unuo = Tarakimu 1, kipengele cha msingi cha hesabu, idadi ya msingi (Mfano mita, kilogramu, ampea nk)
- du → duo = tarakimu 2, jozi, kundi la vitu viwili
- dek du → dek-duo aŭ dekduo = namba 12, kundi la vitu 12
- du mil kvincent → du-mil-kvincento (afadhali si dumilkvincento)
- Mi aĉetis dekon da ovoj kaj dek-duon da pomoj. - Nilinunua mayai kumi na dazeni ya tofaa.
Mchanganyiko wa namba
Wakati namba zinachanganywa na nambari katika muundo wa jina kuunda nambari moja, sheria zingine hujiunga. Nambari zinahitajika kuwa wasifu wa jina la msingi, wakati nambari iliyo katika mfumo wa majina wenyewe ni maneno ya msingi pamoja msemo na da baada yake. Kwa kawaida, suluhisho sahihi ni kutumia da katika matukio haya, kwa sababu da kutumika pamoja na namba si kawaida, ila ni sahihi kabisa.
-
Tie loĝas 1.500.000 homoj. = Tie loĝas unu miliono (kaj) kvincent mil da homoj. - Watu 1,500,000 wanaishi kule.=Milioni moja miatano elfu ya watu wanaishi kule.
Mtu anaweza pia kusema: ...unu kaj duona milionoj da homoj (watu milioni moja na nusu). Au: ... unu komo milionij da homoj (moja mkato tano milioni ya watu).
- Mi havas unu milionon da eŭroj. Se mi ricevos ankoraŭ unu eŭron, mi havos unu milionon unu da eŭroj. - Nina euro milioni. Ikiwa ninapokea euro moja, nitakuwa na euro milioni moja na moja.
- Li havas 10.300.978 $. = Li havas dek milionojn tricent mil naŭcent sepdek ok da dolaroj. - ana $10,300,978= Ana dola milioni kumi mia tatu elfu mia tisa na sabini na nane.
-
Ili kostas kvar kaj duonon da dolaroj. - Iliwagharimu dola nne na nusu.
Suluhisho jingine zuri ni: Ili kostas kvar kaj duonan dolarojn (Yanagharimu dol nne na nusu).
Nambari kwenye mfumo wa vivumishi
Ikiwa mwisho A unaongezwa kwa namba, panaundwa kivumishi mbcho kinaonyesha nafasi ya ngazi namba ngazi:
- unua = Nafasi ya kwanza katika ngazi (hana kingine kabla yake)
- dua = katika nafasi ya pili kwa ngazi (kuna moja kabla yake)
- tria = Katika nafasi ya tatu (kuna mbili kabla yake)
- kvara = Katika nafasi ya nne kwenye ngazi (kuna tatu kabla yake)
- deka = Katika nfasi ya kumi kwenye ngazi (kuna tisa kabla yake)
Nambari ngazi hupokea mwisho J na mwisho N kama viivumishi vya kawaida:
- La sepan tagon de la semajno Dio elektis, ke ĝi estu pli sankta, ol la ses unuaj tagoj. - Mungu alichagua siku ya saba kuwa takatifu kuliko siku sita za kwanza.
Ikiwa mwisho wa A unaongezwa kwa namba ya maneno mengi, maneno yote yanaweza kuunganishwa kuwa neno moja, lakini maneno pia yanaweza kubaki kivyake. Kwa hali yoyote, mwisho A unawekwa tu mwisho. Ikiwa fomu ya pamoja imetumiwa, vistariungio vinawekwa kwa kuweka wazi. Kistariungio kinawekwa pale ambpo kuna nafasi katika namba ya awali ya maneno mengi:
-
Hodiaŭ estas la dudek sepa (tago) de Marto. = ...dudek-sepa... - Leo ni siku ya ishirini na saba ya Machi = ...dudek-sepa... (ya ishirini na saba ...)
(au ...dudeksepa...)
-
Georgo Vaŝington estis naskita la dudek duan de Februaro de la jaro mil sepcent tridek dua. = ...dudek-duan... mil-sepcent-tridek-dua. - George Washington alizaliwa tarehe ya ishirini na mbili Februari mwaka 1732.
Badala ya dudek-duan unaweza pia kuandika dudekduan, lakini badala ya mil-sepcent-tridek-dua usiandike * milsepcenttridekdua * { 2}, kwa sababu hiyo itakuwa sio wazi sana.
- Tio okazis en la okdekaj jaroj. = ...iam en la jaroj de 1980 ĝis 1989 inkluzive. - Hii ilitokea miaka ya themanini. = ... wakati mwingine katika kipindi cha miaka ya 1980 hadi 1989.
-
Ŝi estas la dua plej bona en nia klaso, kaj mi estas la tria. - Yeye ni wa pili kwa ubora katika darasa letu, na mimi ni wa tatu.
Mmoja tu yupo bora kuliko sisi.
Wakati ngazi hutumiwa pamoja na namba ngazi, maelezo ya ngazi yanapaswa kusemwa kwanza kwa uwazi:
-
Tio okazis iam en la unuaj dek tagoj. - Hiyo ilitokea siku moja katika siku kumi za kwanza.
Ikiwa mtu angeweza kusema la dek unuaj tagoj kuna hatari ambayo mtu anaweza kuelewa dek kuwa sehemu ya ngazi, kama la dek-unuaj tagoj.
Maneno mengine ya namba pamoja na mwisho A
Maneno na ON pamoja na mwisho A ni vivumishi vya kawaida.
- duona = Akiwa na nusu tu ya urefu wake kamili.
- triona = Akiwa na sehemu ya tatu tu ya kiasi chake kamili.
- centona = Akiwa na sehemu ya mia moja tu ya kiasi chake kamili.
-
Ĝi estas longa je duona metro. - Ni nusu mita katika urefu.
Ni sentimita 50 za urefu wake.
-
Kvaronan horon li restis. - Walikaa huko kwa muda wa robo saa.
Alibaki dakika kumi na tano.
Miliona (ya milioni), miliarda (ya bilioni), nk ni vivumishi vya kawaida, na inaweza kuwa na maana mbalimbali kulingana na mazingira. Lakini kwa matumizi, maana ya ngazi tu inaonekana: Nia miliona kliento ricevos specialan donacon.
Neno nula ni kivumishi cha kawaida ambacho kinadharia inaweza kutumika kwa maana mbalimbali, kulingana na mazingira, ikiwa ni pamoja na maana ya ngazi: je la nula horo kaj tridek minutoj. Katika matumizi, karibu hutumiwa tu kwa maana "isiyopo, isiyo na maana, batili": Bruo potenca, nula esenco.
Vivumishi vya ngazi kutoka kwa namba zilizochanganywa kinadharia zinazowezekana, lakini karibu hazipendekezwi: nia du-milion-unua kliento. Maneno na numero inapaswa kutumika badala yake: nia kliento numero du milionoj unu.
Namba kwa mfumo wa vielezi
Nambari yenye mwisho E ina maana sawa na sambamba fomu za kivumishi za majibu:
- unue = katika sehemu ya kwanza
- due = katika sehemu ya pili
- dek-due, dek due = katika sehemu ya kumi nambili
- Unue mi redonas al vi la monon, kiun vi pruntis al mi; due mi dankas vin por la prunto; trie mi petas vin ankaŭ poste prunti al mi, kiam mi bezonos monon. - Kwanza ninawapa fedha ambazo umenikopa; pili ninawashukuru kwa mkopo; tatu nakuomba unikopeshe mara nyingine wakati nitahitaji pesa.
- Ĝi estas trione el plasto, trione el ligno kaj trione el metalo. - Sehemu ya tatu ni plastiki, sehemu ya tatu ni mti na sehemu ya tatu ni chuma.
- Tiu monto estas eĉ ne centone tiel alta kiel Ĉomolungmo. = La alteco de tiu monto estas eĉ ne unu centono de la alteco de Ĉomolungmo (= Everesto). - Mlima huu sio hata sehemu ya mia moja kama kwa urefu wa Chomolungma. = Urefu wa mlima huu sio sehemu ya mia moja ya urefu wa Chomolungma (= Mlima Everest).
Matumizi mbalimbali na maneno ya nambari
Vihusishi ĝis, interkajpo vinaweza kutumika na maneno ya nambari kwa kuvitofautisha katika njia mbalimbali:
- Restas ĉirkaŭ dek personoj. = Restas proksimume dek personoj. - Panabaki takribai watu kumi. =Kuna watu wastani kumi wailiobaki.
- Ĝis ducent homoj povas eniri. = Maksimume ducent homoj povas eniri. - Hadi watu mia mbili wanaweza kuingia.= Kiwango cha juu cha watu mia mbili wanaweza kuingia.
- Ili kostas de kvin ĝis dek eŭrojn. = Ili kostas minimume kvin kaj maksimume dek eŭrojn. - Zinauzikana kutoka euro tano hadi kumi. = Zinauzikana angalau euro tano na kiwango cha juu ni euro kumi.
- Mi vidis inter cent kaj ducent homojn. = Mi vidis minimume cent kaj maksimume ducent homojn. - Niliona kati ya watu mia moja na mia mbili. = Niliona angalau mia moja na mia mbili kwa kiwango cha juu.
- Aranĝu ilin en du vicoj, po ses en vico. = Aranĝu ilin en du vicoj, ses en ĉiu vico. - Wapange kwa mistari miwili, sita sita kwa mstari. = Panga kwa mistari miwili, na sita sita kila msitari.
Katika sentensi hizi, vihusishi havihusiki nomino inayofuata, ila zina maana tu kwa idadi. Ikiwa neno la namba limeondolewa, kitofautisho lazima pia kitoweke, kwa sababu haifai tena wala haileti maana.
-
Restas ĉirkaŭ dek personoj. → Restas personoj. - Karibu watu kumi walibakia.→ Watu walibakia
(Restas ĉirkaŭ personojHaina maana.)
-
Mi vidis inter cent kaj ducent homojn. → Mi vidis homojn. - Niliona kati ya watu mia moja na mia mbili watu.→Niliona watu.
(Mi vidis inter homojnhaina maana,)
Vihusishi hivi havionyeshi jukumu katika sentensi wakati vinatofautisha. SI alama ya jukumu, bali vina jukumu la vielezi: ĉirkaŭ = proksimume; de = minimume; ĝis = maksimume.
Maneno yaliyotumiwa kuongeza maelezo ya nambari yanaweza kutumika pamoja na alama za jakumu za kweli, ambazo zinaonyesha jukumu ya maneno yote katika sentensi:
-
Ĝi estis virino, kiu povis havi la aĝon de ĉirkaŭ sesdek jaroj. - Ilikuwa ni mwanamke amabe aiweza kuwa na umri wa miaka wastani wa miaka Sitini.
Ĉirkaŭ inahusu idadi tu sesdek. De inaonyesha jukumu la msemo mzima ĉirkaŭ sesdek jaroj.
-
Nenie en la ĉirkaŭ cent jaroj la loko estis pli ŝanĝita, ol en unu malgranda frukta ĝardeno. - Hakuna mahali ndani ya wastani wa miaka mia moja eneo hilo limebadilika zaidi kuliko kwenye bustani moja ndogo ya matunda.
Adjuct ya wakati ina kihusishi en. Ĉirkaŭ hutoa tu maelezo kwa idadi cent
-
Ili loĝos tie de ok ĝis naŭ jarojn. - Wataishi kule kwa miaka nane mpaka tisa.
Maneno de ok ĝis naŭ jarojn ni adjuct ya muda ambayo lazima iwe na kiashiria cha jukumu. Hapa ina mwisho N. De na ĝis inafanya namba mbali mbali tu.
-
Estis tiel malvarme, ke ili devis kuŝi sub po tri kovriloj. - Ilikuwa hali ya baridi kwa hiyo walijufunika shuka tatu tatu.
Maneno sub po tri kovriloj ni adjuct sub. Po hutoa tu maelezo kwa tri.
-
Li havas ĉirkaŭ mil eŭrojn. - Ana wastani wa euro elfu.
Shamrisho ĉirkaŭ mil eŭrojn inahitaji mwisho N. Ĉirkaŭ inatoa tu maana ya nambari kwa idadi mil.
Katika sentesni hizi, chembe hizi hutumika tu kwa kuongeza maelezo, na hazitumiki kama vihusishi- ukiacha po. Kuhusu po matumizi ya anabadilika. Baadhi hutumia po kila siku kama kihusishi cha kweli, ina maana kamwe mwisho N hautumiwi pamoja napo, hata kama sehemu hiyo ya sentensi huchukua jukumu la shamrisho katika sentensi; kwa mfano, Mi donis al ili po dek eŭroj.Wengine wanatumia po kama kielezi, na wanongeza na mwisho N wakati jukumu lake katika sentensi hiyo linalazimisha, kw mfano Mi donis al ili po dek eŭrojn..Yote matumizi ni sahihi.
Maelezo ya hisabati
Fomula | Neno |
---|---|
2 + 2 = 4 | Du kaj du faras kvar. / Du plus du estas kvar. |
10 – 3 = 7 | Dek minus tri faras sep. |
22 × 6 = 132 | Dudek du multiplikite per ses faras cent tridek du. / Dudekduoble ses estas cent tridek du. / Dudek du oble ses egalas al cent tridek du. |
7:2 = 3,5 | Sep dividite per du faras tri komo kvin. |
46,987 | kvardek ses komo naŭ ok sep (hapana...komo naŭcent okdek sep |
10² = 100 | La dua potenco de dek estas cent. / Dek kvadrate estas cent. |
5³ = 125 | La tria potenco de kvin estas cent dudek kvin. / Kvin kube estas cent dudek kvin. |
- Kvin kaj sep faras dek du. - Tano jumlisha saba sawasawa na kumi na mbili.
- Dek kaj dek faras dudek. - Kumi jumlisha kumi sawasawa ishirini.
- Kvar kaj dek ok faras dudek du. - Nne jumlisha kumi na nane sawsawa na ishirini na mbili.
- Tridek kaj kvardek kvin faras sepdek kvin. - Therathini kujumlisha arobaini na tano hufanya Sabini na tano.
- Kvinoble sep estas tridek kvin. - Tano mara Saba sawsawa na thelathini na tano.
Alama ya sawasawa(=) inaweza kutamkwa kamafaras (hufanya) au estas(ni)auegalas (al) (sawasawa[kwa]), au zaidi kwa upendeleo wa msemaji: du kaj du faras kvar, dek minus tri estas sep, du oble du egalas (al) kvar.
Usitumie nukta badala ya mkato ikiwa ni desimali. Nukta hutumiwa kama alama ya desimali katika nchi fulani. Lakini Kiesperanto,kama nchi nyingine zingine nyingi na lugha zingine, kinatumia mkato na desimali.
Fomula | Neno |
---|---|
9403,5 km | naŭ mil kvarcent tri komo kvin kilometroj / naŭ mil kvarcent tri kaj duona kilometroj |
8,6 kg | ok komo ses kilogramoj / ok kilogramoj (kaj) sescent gramoj |
+37,7° | (plus) tridek sep komo sep gradoj / tridek sep komo sep gradoj super nulo |
49,75 USD | kvardek naŭ komo sep kvin (Usonaj) dolaroj / kvardek naŭ (Usonaj) dolaroj (kaj) sepdek kvin cendoj |
Maneno ya sehemu kma gramoj (grama) na cendoj (senti) unaweza kuyasikia kwa mbali mmuda mwingine katika maelezo kama haya:tri kilogramoj (kaj) sepcent, kvar dolaroj (kaj) sepdek kvin. Mzungumzaji anapaswa kuwa mwangalifu kuwa na uhakika kwamba hakuna tatizo wala shaka kuhusu sehemu ya aina gani inasemwa.
Saa
Ili kuonyesha saa, moja ya mifano zifuatazo zinapaswa kutumika. Maneno horo (saa) na minutoj (dakika) mara nyingi huasikika tu.
Kitarakimu | Kwa msemo |
---|---|
3:15 (aŭ 15:15) | Estas la tria (horo) (kaj) dek kvin (minutoj). / Estas dek kvin (minutoj) post la tria (horo). |
9:45 (aŭ 21:45) | Estas la naŭa (horo) (kaj) kvardek kvin (minutoj). / Estas dek kvin (minutoj) antaŭ la deka (horo). |
Ili kuongeza usahihi zaidi, maelezo {1 en la antaŭtagmezo au antaŭtagmeze (asubuhi), na en la posttagmezo au posttagmeze (katika mchana) inaweza kuongezwa. Lakini mfumo wa masaa 24 pia unaweza kutumika:
- Estas la dek-kvina (kaj) dek kvin. / Estas dek kvin post la dek-kvina. - Ni saa tisa za jioni na dakika kumi na tano.
- Estas la dudek-unua (kaj) kvardek kvin. / Estas dek kvin antaŭ la dudek-dua. - Ni saa tatu za usiku na dakika arobaini na tano
Badala ya 15 minutoj (dakika 15), unaweza kusema kvarono (robo), kvaronhoro (robo saa) au kvarona horo (robo saa). Badala ya 30 minutoj (dakika 30), wanatumia mara nyingi duono (nusu), duonhoro (nusu saa), au duona horo ( nusu saa).
Mtu huongea kuhusu saa kwa kutumia namba ngazi: tria (ya tatu), naŭa (ya tisa), dek-dua (kumi na mbili), nk. Ukitaka kuuliza sa unatumia neno la swali kiom (kiasi gani) + mwisho A kioma{2 } (ni ngapi)
- kiom? - Ni kiasi gani? Ni ngapi? → tri, naŭ, dek du, dudek unu...
- kioma? - Ni yangapi? → tria, naŭa, dek-dua, dudek-unua...
- Kioma horo estas, gardisto? - Ni saa ngapi, mlinzi?
- Kioma horo estis, kiam vi alvenis? - Ilikuwa ni muda gani wakati ulipofika?
Kuonyesha wakati kitu kinatokea, kiashiria cha jukumu inapaswa kutumika, kwa kawaida je, antaŭ, post, ĝis aŭ ĉirkaŭ:
- Je (la) kioma horo okazis tio? - Ni saa ya ngapi ile ilipotokea? Ilikuwa ni muda gani ilipotokea?
- Tio okazis je la tria kaj kvardek. - Ile ilitokea saa tisa na dakika arobaini. Ilitokea saa tisa na dakika arobaini (3:40)
- Ni devas manĝi antaŭ la oka. - Tutapaswa kula kabla ya saa mbili.
- Post la dek-unua horo ĉio devas esti preta. - Baada ya saa tano, kila kitu kitakuwa tayari.
Wakati wa kutaja saa, kiashiria N hakitumiwi kwani kuna uwezekano wa kuchanganya saa na tarehe ambayo inaoneshwa ukitumia namba ngazi: je la tria = "je la tria horo", la trian = "en la tria tago de la monato".
Tarehe
Mifano ifuatazo inapaswa kutumika kuonyesha tarehe. Maneno tago (siku) na en la jaro (mwaka) mara nyingi husikik kwa mbali.
- Estis la tria (tago) de Decembro (en la jaro) mil naŭcent naŭdek unu. - Ilkuwa siku ya tatu (siku) Desemba (mwaka) elfu moja mia tisa tisini na moja.
- Hodiaŭ estas la dua (tago) de Majo (en la jaro) du mil kvin. - Leo ni siku ya pili(siku) ya Mei (mwaka) elfu mbili na tano.
- Morgaŭ estos la dudek kvina (tago) de Julio (en la jaro) du mil dek. - Kesho itakuwa ni tarehe Ishirini na tano (siku) Julai (mwaka) elfu mbili na kumi.
Nambari za kawaida zinaweza pia kutumika kwa miaka, lakini matumizi haya yanakuwa machache: Estis la lasta de Januaro (en la jaro) mil-okcent-okdek-sepa.
Kati ya siku na mwezi, de (ya) inapaswa kutumiwa daima, kwa sababu namba ngazi haihusiani na mwezi, lakini na neno tago (siku), ambalo kawaida huachwa: la unua de Majo = la unua tago de Majo, la dek-tria de Decembro = la dek-tria tago de Decembro. Ukisema la unua Majo inamaanisha Mei ya kwanza miongoni miezi kadhaa ya Mei.
Ili kuonyesha tarehe wakati kitu kilitokea, kinatokea, au kitatokea, kiashiri kinatumika. mwisho N mara nyingi hutumiwa kwa kusudi hili:
- Ili venos la sepan (tagon) de Marto. = Ili venos en la sepa (tago) de Marto. - Watakuja siku ya saba Machi.= Watakuja siku ya saba ya Mwezi wa Tatu.
- La unuan de Majo ili komencis sian vojaĝon. = En la unua (tago) de Majo... - Tarehe mosi Mei walianza safari yao. = Siku ya kwanza ya Mei ...
Mi laboris tie ĝis la unua de Aŭgusto mil naŭcent sesdek. - Nilifanya kazi kule mpaka tarehe mosi ya Ogasti mwaka elfu moja na mia tisa na sitini.
- Antaŭ la lasta tago de Junio vi devas trovi laboron. - Kabla siku ya mwisho ya Juni unatakiwa kupata kazi.
- Post la dek kvina de Marto ŝi loĝos ĉe mi. - Baada ya tarehe kumi na tano ya Machi ataishi na nyumbani kwangu.