Kwa maudhui

Kihusishi de kin maana nyingi. Kwa sababu ya wingi wa maana yake, wakati mwingine unaweza kuwa na mashaka. Unaweza kisha kuongeza maelezo tofauti au kuchagua kihusishi kingine.

hatua, mwendo, harakati

Maana ya msingi ya kihusishi de ni mahali ambapo hatua huanza:

  • Mi venas de la avo, kaj mi iras nun al la onklo. - Nimekuja kutoka kwa babu, na sasa ninaenda kwa mjomba.
  • La vento forblovis de mia kapo la ĉapon. - Upepo ulirusha kofia yangu kutoka kwenye kichwa changu.
  • Ilia vojaĝo de Delhio al Kalkato estis tre longedaŭra. - Safari yao kutoka Delhi hadi Kalkato ilikuwa ndefu sana.
  • Rekta linio estas la plej mallonga vojo de unu punkto al alia. - Mstari mnyoofu ni njia fupi kutoka sehemu moja hadi nyingine.
  • For de tie ĉi! - Mbali na hapa!

Kwa usahihi, unaweza kutumia for de au disde: polisi wametoa fedha zilizoibiwa kutoka kwa jambazi / disde la rabisto . Ikiwa mtu anaweza kusema: ...la ŝtelitan monon de la rabisto}, mtu anaweza kufikiri kuwa ni mali } ya : "... fedha iliyoibiwa ambayo ilikuwa ya jambazi."

Mwanzo/chimbuko, sababu

De pia inaweza kuonyesha asili/chimbuko au sababu:

  • De la patro mi ricevis libron, kaj de la frato mi ricevis plumon. - Nilipokea kitabu kutoka kwa baba na nilipokea kalamu kutoka kwa ndugu.
  • La hebreoj estas Izraelidoj, ĉar ili devenas de Izraelo. - Waebrania ni Waisraeli kwa sababu walitoka kwa Israeli.
  • Francisko de Asizo = huyo Francisco, ambayo anatoka mjini Asizo = Francisko el Asizo - Francisco wa Assisi
  • Li paliĝis de timo kaj poste li ruĝiĝis de honto. = ...pro timo... pro honto. - Alififia kwa hofu na kisha akawa mwekundu kwa aibu. = ... kwa hofu ... kwa aibu.

    Kwa sababu moja, hata hivyo, unatumia kawaida pro na wakati mwingine el.

  • Ebria de feliĉo, mi alkroĉiĝis al lia kolo. - Mlevi wa furaha, nikamfunga shingo yake.

Tofauti k.s

De mara nyingi huonyesha utofauti, kutengwa, umbali, kutawanyika:

  • Mi povus diferencigi la saĝajn de la malsaĝaj! - Ningeweza kutofautisha hekima na upumbavu.
  • Kial Vi kaŝas vin de mi? - Kwanini unajificha kwangu?
  • Nun mi iom liberiĝis de la plej urĝaj el miaj kolektiĝintaj laboroj. - Sasa nimejitoa eko baadhi ya kazi za dharula sana kwenye mkusanyiko wa kazi zangu.
  • Ĝi estas libera de malsanoj. - Hakina maradhi.
  • Ili loĝas malproksime de ni. - Wanaishi mbali nasi.

Muda

De pia inaweza kuonyesha wakati wa mwanzo wa hatua inayoendelea au hali:

  • Li laboras de la sesa horo matene. - Hufanya kazi kutoka saa kumi na mbili za asubuhi.
  • De nun mi ne plu manĝos viandon. - Kuanzia sasa sitakula nyama kamwe.
  • Mi konas lin de longa tempo. - Nimemjua kwa muda mrefu (na bado namjua).

Kwa kuonyesha vizuri kama ni muda, unaweza kutumiaekde au de post:

ekde
=kutoka mwanzo wa
de post
=kutoka mwisho wa

Ikiwa inahusu muda, ni kama hakuna tofauti kati ya ekde kaj de post, lakini ikiwa kipindi cha muda, tofauti ni kubwa: de post ŝia vivo (baada ya maisha yake) = ekde ŝia morto (tangu kifo chake)

umilikaji

Mara nyingi de huonyesha mali (= milki, matazamio, ukaribu, uhusiano, ushirikiano, undugu ...):

  • Jen kuŝas la ĉapelo de la patro. - Ona kofia ya baba ipo.

    Baba ndiye mmiliki wa kofia Kofia kama miliki au mali.

  • La dentoj de leono estas akraj. - Meno ya simba ni makali.

    Meno yanamilikiwa na simba kama sehemu ya mwili wake.

  • Sur la bordo de la maro staris amaso da homoj. - Kwenye kando ya bahari palisimama umati wa watu.

    Kando inamilikiwa na bahari, kwa sababu inapatikana karibu yake.

  • Januaro estas la unua monato de la jaro. - Januari ni mwezi wa kwanza wa mwaka.

    Miezi ni sehemu za mwaka.

  • La filo de la reĝo ŝin renkontis. - Kijana wa Mfalme alimkuta.

    Kijana anamilikwa na Mfalme kama anavyohusiana naye.

  • Mi legos poemon de Zamenhof. - Nitasoma kishairi cha Zamenhof.

    Kishairi kinamilikiwa na Zamenhof kwasababu alikitunga.

  • Glaso de vino estas glaso, en kiu antaŭe sin trovis vino, aŭ kiun oni uzas por vino. - Glasi ya divai ni glasi ambayo hapo awali ilikuwa na divai, au ambayo hutumiwa kwa divai.

    Glasi ni ya divai na divai kwasababu imetengwa kwa kutumiwa kwa divai.

  • Ŝi estas profesoro de matematiko. - Ni profesa wa a hisabati.

    Profesa anamilikiwa na hisabati kwasababu ni hiyo ni kazi yake. Unaweza pia kutumiapri.

  • Tiu libro estas de Karlo. - Kitabu kile ni cha Karlo.

    Mara nyingi tunatumia aparteni + al : Tiu libro apartenas al Karlo.

  • Ĝi estas de mi. - Niyakwangu.

    Kwa kawaida tunasemaĜi estas mia. Ĝi apartenas al mi.

Kiima, mtendaji, shamrisho

Msemo na De, ambayo nyongeza kwa nomino, inaonyesha kawaida kiima chenye maana (mtendaji) au shamrisho ya maana ya kitendo:

  • La kanto de la birdoj estas agrabla. - Wimbo wa ndege unafurahisha.

    Ndege wanaimba.

  • Li tuj faris, kion mi volis, kaj mi dankis lin por la tuja plenumo de mia deziro. - Hraka alifanya kile ambacho nilihitaji na nakamshukuru kwa utimilifu wa haraka wa mahitaji yangu.

    Alitimiza mahitaji yangu.

Kuangalia kama ni kiima tunaweza kutumia fare de:Hodiaŭ posttagmeze okazos akcepto fare de la urbestro. (Leo mchana kuna mapokezi yatakayofanywa na meya)

Angalia: Watu wengine hufupisha far de kwa far, lakini neno hilo halijulikani na halipendekezi kwa matumizi.

Kuhusu kauli ya kutendewa, de mara nyingi huonyesha kiima, mtendaji:

  • Ŝi estas amata de ĉiuj. - Anapendwa na wote.

    (wao)Wote wanampenda.

  • Li estis murdita de nekonato. - Aliuawa na asiyejulikana (mshambuliaji).

    Mtu asiyejulikana alimuua.

  • La montoj estis kovritaj de neĝo. - Milima ilifunikwa na theruji.

    Theruji ilifunika milima.

Unaweza pia kutumia fere de: La infano estis forprenita fare de la patrino (Mtoto ulibebwa na mama yake) . Lakini de ya kawaida hutosha kwenye kauli ya kutendewa. Ikiwa maana nyingine huhitajika kwa de kwa kauli ya kutendewa, basi mara nyingi ni muhimu kuliyonyesha vizuri kwa kutumia disde, for de, { 1} ekde au kitu kama hicho: La infano estis forprenita disde la patrino. (Mtoto aliachanishwa na mama yake) (Walimbeba mbali na mama yake.)

Ubora

De wakati mwingine inaonyesha ubora, muundo, au kipimo:

  • Ŝi estas virino de meza aĝo. = Ŝi estas mezaĝa virino. - Ni mwanamke wa umri wa kati=Ni mwanamke wa umri wa kati.
  • Li havas harojn de nedifinita koloro. - Ana nywele za rangi isiyojulikana.
  • Li estas de meza kresko. - Yuko kwenye wastani wa urefu.
  • bukedo de rozoj = shada la maua ya waridi
  • reto de komputiloj = Mtandao(kazi) ambayo ina kompyuta
  • La knabo havis aĝon de nur ses jaroj. - Kijana alikuwa naumri wa miaka Sita tu.(Kijana alikuwa na umri wa miaka Sita)
Kurudi juu