Kwa maudhui

Vivumishi vinaonyesha tabia, sifa, mali, mahusiano, nk. Vivumishi katika Kiesperanto mwisho wake ni -A

  • longa - refu = chenye urefu mkubwa
  • ruĝa - nyekundu = chenye sifa ya wekundu
  • bona - zuri/ema = inayojulikana kwa sifa nzuri
  • inteligenta - erevu = chenye au mwenye kuwa na werevu, inayojulikana kwa werevu
  • homa - -a kibinadamu = wanaohusishwa na mtu
  • malaperinta - kilicho kosekana/kilichopotea = hivyo tayari kimepotea

Pia posedaj pronomoj na maneno ya namba ngazi ni vivumishi, lakini kwa maneno haya mwisho -A una maana maalum.

Baada ya mwisho -A panaweza kufuata -J alama ya wingi, na mwisho wa accusative -N. Unaweza pia kuweka zote mbili, lakini daima J kabla ya N:

longaj longan longajn
ruĝaj ruĝan ruĝajn
miaj mian miajn
sesaj sesan sesajn

Kwa kulinganisha vivumishi vinatumiwa pamoja na tumaneno pli na plej.

Matumizi ya vivumishi

Vivumishi hutumiwa hasa kuelezea nomino.

Vivumishi vya wasifu

Vivumishi vinaweza kutumika kama wasifu wa nomino (kuelezea moja kwa moja vivumishi). Vivumishi vya wasifu kawaida vinakuja kabla ya jina, lakini pia vinaweza kuja baada yake. Kunaweza pia kuwa na vivumishi kwa wakati mmoja kabla na baada ya jina moja:

  • granda domo - nyumba kubwa
  • domo granda - nyumba kubwa
  • la tago longa - siku ndefu
  • la longa tago - siku ndefu
  • fama Franca verkisto - Mwandishi maarufu mfaransa
  • fama verkisto Franca - mwandishi maarufu wa mfaransa
  • Lingvo Internacia (la origina nomo de Esperanto) - Lugha ya Kimataifa (jina la awali la Kiesperanto)

Vivumishi wasifu ambavyo vinasimama baada ya jina lake, mara nyingi kwa kusisitizwa.

vivumishi vya prediketo

Kivumishi kinaweza kuelezea kitu predikative, pere de verbo:

  • La domo estas granda. - Nyumba ni kubwa.

    Granda inaelezea jina domo kwa kutumia kitenzi estas.

  • Tiuj ĉi verkistoj iam iĝos famaj. Waandishi hawa wakati mmoja watakuwa maarufu.

    Famaj inaelezea nomino verkisto kwa kuwa kutumiaiĝos .

  • Mi farbis mian domon blanka. Niligeuza nyumba yangu nyeupe.

    Blanka inaelezea nomino domon kwa kutumia kitenzi farbis .

Uelezaji wa maneno mengine

Vivumishi pia hutumiwa kuelezea tumaneno tuliyo tumika kama nomino, kwa mfano personajn pronomojn, kwa kawaida preketo:

  • Mi estas feliĉa. - Nina furaha.
  • Tiu estas mia. - Hii ni yangu.
  • Tio estas bona. - Hiyo ni nzuri.
  • Ili fariĝis koleraj. - Walikasirika.
  • Ambaŭ ŝajnis dormantaj. Wote(wawili) walionekana wamelala.

Matumizi kama nomino ya vivumishi

Wakati kivumishi kinatumika kama wasifuya jina, wakati mwingine jina linaachwa. Kisha kivumishi kinakuwa kama kinachukua kazi ya jina. Hii inawezekana wakati muktadha unaonyesha kwa wazi kwamba jina linapaswa kueleweka kidogo:

  • La palaco de la imperiestro estis la plej belega [palaco] en la mondo.

    Ikulu kwa mfalme kulikuwa pazuri zaidi duniani.

  • Mi ne volas tiun ĉi supon, donu al mi alian [supon].

    Sitaki supu hii, nipe nyingine [supu].

  • Tro malmultaj [homoj/aŭskultantoj] venis.

    [watu / wasikilizaji] wachache sana walikuja.

  • Kelkaj [personoj] el ni alvenis malfrue.

    Baadhi ya watu [wetu] miongoni mwetuwalifika wamechelewa.

  • Ni ambaŭ volas la saman [aferon]. (Aŭ: Ni ambaŭ volas la samon.)

    Sisi wote (wawili) tunataka kitu kimoja.

  • Vi estas la unuaj [personoj], kiujn mi vidas hodiaŭ matene.

    Nyinyi mko watu wa kwanza ambao ninaona leo asubuhi.

  • Via pano estas malpli freŝa, ol mia [pano].

    Mkate wako ni kukuu kuliko [mkate] wangu.

  • Estas nun la dua [horo].

    Sasa ni saa nane.

  • Mi parolas la Francan [lingvon].

    Ninazungumza Kifaransa [lugha].

Tumaneno tulitumika kama kivumishi

Baadhi ya tumaneno katika Kiesperanto tunaweza kuwa kama vivumishi kwenye sentensi, lakini hatuna mwisho A, U, ES , neno ambaŭ na namba .

  • Tiun straton mi neniam vidis antaŭe.

    Sikujawahi kuona barabara hiyo kabla.

  • Mi korektis ambaŭ erarojn.

    Nilikosowa makosa yote mawili.

  • Tie loĝas du Hungaroj kaj tri Kanadanoj.

    Pale panaishi raia wawili wa Hungari na wakanada watatu.

Kurudi juu